Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi

Walikuwa macho ya Israeli kwenye mpaka - lakini tahadhari zao kuhusu Hamas hazikusikika

 


Female soldiers who guarded Israel's border
  • Author,Alice Cuddy
  • Nafasi,BBC News, Israel

Wanajulikana kama macho ya Israeli kwenye mpaka wa Gaza.

Kwa miaka mingi, vitengo vya vijana wa kike walioandikishwa kujiunga na jeshi vilikuwa na kazi moja hapa. Ilikuwa ni kukaa katika vituo vya uchunguzi kwa saa nyingi, kutafuta dalili za kitu chochote cha kutiliwa shaka.

Katika miezi kabla ya mashambulizi ya 7 Oktoba ya Hamas, walianza kuona mambo: mazoezi ya kufanya uvamizi, utekaji nyara , na wakulima kuwa na tabia ya ajabu katika upande mwingine wa ua.

Noa, sio jina lake halisi, anasema wangepitisha habari kuhusu kile walichokuwa wakikiona kwa maafisa wa ujasusi na wa ngazi za juu, lakini hawakuwa na uwezo wa kufanya zaidi. "Tulikuwa macho tu," anasema.

Ilikuwa wazi kwa baadhi ya wanawake hawa kwamba Hamas ilikuwa inapanga jambo kubwa - kwamba kulikuwa na, kwa maneno ya Noa, "puto ambalo lingepasuka".

BBC sasa imezungumza na wasichana hawa kuhusu kuongezeka kwa shughuli za kutiliwa shaka walizoziona, ripoti walizowasilisha, na kile walichokiona kama ukosefu wa majibu kutoka kwa maafisa wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF).

Tumeona pia ujumbe wa WhatsApp ambao wanawake walituma miezi kabla ya tarehe 7 Oktoba, wakizungumza juu ya matukio kwenye mpaka. Kwa baadhi yao ikawa utani wa giza: ni nani angekuwa zamu wakati shambulio lisiloepukika lilikuja?

Sio wanawake hawa pekee waliotoa hofu, na kadiri ushuhuda unavyokusanywa, hasira dhidi ya taifa la Israel - na maswali juu ya majibu yake - yanaongezeka.

BBC imezungumza pia na familia zinazoomboleza ambazo sasa zimepoteza binti zao, na wataalamu ambao wanaona majibu ya IDF kwa wanawake hawa kama sehemu ya kushindwa kwa idara za ujasusi. IDF ilisema "kwa sasa inalenga katika kuondoa tishio kutoka kwa shirika la kigaidi la Hamas" na ilikataa kujibu maswali ya BBC.

"Tatizo ni kwamba wao [wanajeshi] hawakuunganisha nukta," kamanda wa zamani katika kitengo kimoja cha mpaka aliambia BBC.

Kama wangekuwa, anasema, wangegundua kuwa Hamas ilikuwa ikitayarisha kitu ambacho hakijawahi kutokea.

Shai Ashram, 19, alikuwa mmoja wa wanawake waliokuwa zamu tarehe 7 Oktoba. Katika simu na familia yake, ambapo waliweza kusikia milio ya risasi ikilia kwa nyuma, alisema kulikuwa na "magaidi kwenye kambi hiyo na kwamba kutakuwa na tukio kubwa sana".

Alikuwa mmoja wa askari zaidi ya kumi na wawili waliouawa. Wengine walichukuliwa mateka.

Shai Ashra, posing with hands on hips, in military fatigues
Maelezo ya picha,

Shai Ashram - baba yake anasema alipenda kuwa mwanajeshi

Hamas iliposhambulia, wanawake wa Nahal Oz, kituo kilicho karibu kilomita moja kutoka mpaka wa Gaza, walianza kuagana kwenye kundi lao la WhatsApp la pamoja.

Noa, ambaye hakuwa zamu na alikuwa akisoma jumbe kutoka nyumbani, anakumbuka kuwaza "hili ndilo". Shambulio ambalo walikuwa wakihofia kwa muda mrefu sasa lilikuwa linatokea.

Kwa sababu ya maeneo ya vituo vyao, wanawake wa kitengo hiki cha kijeshi - kinachojulikana kama tatzpitaniyot kwa Kiebrania - walikuwa miongoni mwa Waisraeli wa kwanza ambao Hamas ilifikia baada ya kutoka Gaza.

"Kazi yetu ni kulinda wakazi wote"

Wanawake hao huketi ndani ya vyumba vilivyo karibu na mpaka, wakitazama kwa saa nyingi kila siku picha za uchunguzi wa moja kwa moja zilizonaswa na kamera kando ya uzio wa teknolojia ya juu, na puto zinazoelea juu ya Gaza.

Kuna vitengo kadhaa vya hivi karibu na uzio wa Gaza, na vingine katika nafasi tofauti kwenye mipaka ya Israeli. Vyote vinawasheheni wanawake wachanga, wenye umri wa miaka ya mwisho ya utineja hadi miaka ya mwanzo wa 20. Hawabebi bunduki.

Katika wakati wao wa mapumziko, wanawake vijana wangejifunza taratibu za kucheza dansi, kupika chakula cha jioni pamoja, na kutazama vipindi vya televisheni. Kwa wengi, wakati wao katika jeshi ilikuwa mara yao ya kwanza kuishi mbali na familia zao, na wanaelezea kuunda uhusiano kama wa dada katika familia.

Lakini wanasema walichukua majukumu yao kwa uzito. "Kazi yetu ni kulinda wakazi wote. Tuna kazi ngumu sana - unakaa kwenye zamu na hauruhusiwi kupepesa macho au kusogeza macho yako hata kidogo. Lazima uwe na umakini kila wakati," Noa anasema.

Makala iliyochapishwa na IDF mwishoni mwa Septemba inaorodhesha tatzpitaniyot pamoja na vitengo vya kijasusi vya jeshi la Israeli kama vile "vinavyojua kila kitu kuhusu adui".

Wanawake hao wanapoona kitu cha kutiliwa shaka hukiwasilisha kwa kamanda wao na kwenye mfumo wa kompyuta ili kutathminiwa na maafisa wakuu zaidi.

TH

Meja Jenerali Mstaafu wa IDF Eitan Dangot anasema tatzpitaniyot ina jukumu kubwa katika "kubonyeza kitufe kinachosema kuwa kuna kitu kibaya", na kwamba wasiwasi wanaoibua na kamanda unapaswa kupitishwa "ili kuunda picha ya kijasusi".

Anasema uangalizi wao muhimu hujaza 'vipande vya mafumbo' katika kuelewa vitisho yoyote.

Katika miezi kadhaa kabla ya mashambulizi ya Hamas, maafisa wakuu wa Israel walitoa taarifa kwa umma wakipendekeza kuwa tishio la Hamas lilikuwa limedhibitiwa.

Lakini kulikuwa na ishara nyingi kwenye mpaka kwamba kuna kitu kibaya sana.

Mwishoni mwa Septemba, mtazamaji huko Nahal Oz anaandika katika kikundi cha marafiki cha WhatsApp kwenye kitengo: "Kuna tukio gani lingine?"

Jibu la haraka kupitia sauti lilisema: "Msichana, umekuwa wapi? Tumekuwa na tukio moja kila siku kwa wiki mbili zilizopita."

Maoni tunayozungumza ili kuelezea matukio kadhaa waliyoona kwa wakati halisi katika miezi kabla ya tarehe 7 Oktoba, na kusababisha baadhi ya watu kuwa na wasiwasi kwamba shambulio lilikuwa linakuja.

"Tungewaona wakifanya mazoezi kila siku jinsi uvamizi huo ungekuwa," Noa, ambaye bado anahudumu katika jeshi, aliambia BBC. "Hata walikuwa na kifaru cha mfano ambacho walikuwa wakifanya mazoezi ya jinsi ya kukichukua.

"Pia walikuwa na mfano wa silaha kwenye uzio na pia wangeonyesha jinsi watakavyolipua, na kuratibu jinsi ya kuchukua vikosi na kuua na kuteka nyara."

Eden Hadar, mtazamaji mwingine kutoka kituo hicho, anakumbuka kwamba mwanzoni mwa huduma yake, wapiganaji wa Hamas walikuwa wakifanya mafunzo ya mazoezi ya kimwili katika sehemu aliyoitazama. Lakini katika miezi kadhaa kabla ya kuondoka jeshini mnamo Agosti, aliona mabadiliko ya "mafunzo halisi ya kijeshi".

TH

Katika kituo tofauti mpakani, Gal (sio jina lake halisi), anasema pia alikuwa akitazama jinsi mafunzo yalivyoongezeka.

Alitazama, kupitia puto ya uchunguzi, kama kielelezo cha silaha ya kiotomatiki ya Israeli kwenye mpaka ikijengwa "katikati ya Gaza", anasema.

Wanawake kadhaa pia wanaelezea mabomu yaliyokuwa yametegwa na kulipuliwa karibu na uzio huo - unaojulikana kama Ukuta wa chuma wa Israel - inaonekana kujaribu nguvu zake. Picha za tarehe 7 Oktoba baadaye zingeonyesha milipuko mikubwa kabla ya wapiganaji wa Hamas kukimbia kwa pikipiki.

Kwa mtazamaji wa zamani Roni Lifshitz, ambaye alikuwa bado anahudumu lakini hafanyi kazi wakati Hamas iliposhambulia, jambo lililompa wasi wasi zaidi aliloliona katika wiki zilizopita ni doria ya mara kwa mara ya magari yaliyojaa wapiganaji wa Hamas, ambayo yangesimama kwenye vituo vya kutazama upande wa pili wa ua.

Roni Lifshitz pictured seated, wearing military fatigues
Maelezo ya picha,

Roni Lifshitz anasema aliona wanaume wakipiga picha za uzio kutoka upande wa Gaza

Anakumbuka wanaume "wakizungumza, wakionyesha kamera na uzio, wakipiga picha".

Anasema aliweza kuwatambua kuwa wanatoka katika Kikosi cha Hamas cha Nukhba kwa sababu ya mavazi yao. Israel imesema hii ilikuwa mojawapo ya "vikosi vilivyoongoza" mashambulizi ya Oktoba.

Simulizi ya Roni inalingana na ya mwanamke mwingine katika kituo hicho ambaye alizungumza na BBC.

Emoji za Moyo na GIF

Baadhi ya walinzi pia wanazungumza juu ya kuongezeka kwa matukio ya majaribio ya uvamizi.

Jumbe zinazoshirikiwa nasi na mwanajeshi mmoja wa kike zinarejelea kwa kificho gari za kubebea mizigo kwenye mpaka, na pia IDF inayowazuia watu wanaojaribu kuvuka kuingia Israel, jambo ambalo anasema lilikuwa likitokea mara kwa mara. Wanachama wa kitengo wanapongezana kwa kuzuia hili kwa emoji za moyo na GIF.

Katika ujumbe mchunguzi Shahaf Nissani aliotuma kwa mama yake mwezi Julai, anaandika: "Habari za asubuhi mama. Nilimaliza zamu sasa na tulikuwa na [jaribio la watu kuingia mpakani] lakini tukio hili lilikuwa la kusisimua sana ... kana kwamba lilikuwa tukio ambalo hakuna aliyewahi kukutana nalo."

Wanawake pia walianza kuona mabadiliko ya ajabu katika mifumo ya tabia mpakani.

Wakulima wa Gaza, wakamata ndege na wachungaji wa kondoo walianza kusogea karibu na uzio wa mpaka, wanasema. Waangalizi sasa wanaamini kuwa watu hawa walikuwa wakikusanya taarifa za kijasusi kabla ya mashambulizi hayo.

An observation tower operated by Hamas at a position along the border with Israel

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mnara wa uchunguzi unaoendeshwa na Hamas katika eneo la mpaka na Israel

Palestinian shepherds walk with their sheep, east of Gaza City near the border with Israel

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Waangalizi wa Israel wanasema walianza kuona nyuso zisizojulikana huko Gaza kabla ya shambulio la Hamas

"Tunamfahamu kila mmoja kwa sura na tunajua kwa hakika utaratibu na saa zake. Ghafla tulianza kuwaona washikaji ndege na wakulima tusiowajua. Tumewaona wakihamia maeneo mapya. Utaratibu wao umebadilika," anasema mwangalizi Avigail, ambaye aliomba kutotajwa ili kuongea juu ya kile alichokiona.

Noa pia anawakumbuka wakikaribia "karibu zaidi" na uzio.

"Washika ndege wangeweka vizimba vyao kwenye uzio, inashangaza kwa sababu wanaweza kuviweka popote, wakulima pia wangeshuka karibu kabisa na uzio katika eneo ambalo si la kilimo na hakuna sababu zaidi ya kukusanya taarifankuhusu mfumo huo na kuona jinsi wanavyoweza kuupita. Ilitupa wasi wasi sana," anasema.

"Tulizungumza juu ya hayo wakati wote."

Sio kila mtu tuliyezungumza naye alikuwa anajua umuhimu wa kile walichokuwa wakikiona.

Hamas daima ilikuwa ikijinoa kwa ajili ya mashambulizi, na baadhi ya wanawake hawakutarajia kwamba ilikuwa ikijiandaa kwa lolote katika kiwango cha tarehe 7 Oktoba, mmoja alisema.

Waangalizi kadhaa ambao walihofia shambulio kubwa lingekuja wameambia BBC kuwa wanahisi wasiwasi wao haukusikilizwa.

Alipogundua magari hayo mpakani, Roni anasema itifaki ilikuwa ni kumtahadharisha kamanda wake na kisha kuendelea kutazama hadi magari yasiwe tena katika sehemu yake. Kisha angeiweka katika mfumo wa kompyuta ambapo "itapitishwa" kwenda kwa maafisa wa ngazi ya juu.

Lakini, anasema, "hajui" ripoti hizi zilienda wapi.

"Labda kwa idara ya ujasusi lakini ikiwa wanafanya kitu nayo au la, sijui," anasema. "Hakuna aliyetupa jibu kuhusu yale tuliyoripoti na kuwasilisha."

Noa anasema hakuweza kuhesabu ni mara ngapi alikuwa amewasilisha ripoti. Ndani ya kitengo, kila mtu "aliichukulia kwa uzito na angeipitisha lakini mwisho wao [watu walio nje ya kitengo] hawakufanya chochote kuihusu".

TH

Avigail anasema kwamba hata maafisa wakuu walipokuja kwenye kituo hicho "hakuna mtu ambaye angezungumza nasi au kuuliza maoni yetu au kutuambia kidogo juu ya kile kilichokuwa kikiendelea".

"Walikuja tu, wakatupa majukumu na kuondoka," anasema.

'Kwa nini tuko hapa ikiwa hakuna mtu anayesikiliza?'

Kama kamanda katika kitengo chake, Gal anasema waangalizi wangempa taarifa ambazo alizipitisha kwa msimamizi wake.

Lakini anasema kwamba wakati hii ilijumuishwa katika "tathmini ya hali" - wakati viongozi wa ngazi ya juu wangejadili ripoti zilizowasilishwa na waangalizi - hakuna kitu kilichoonekana kufanywa zaidi ya hapo.

Wanawake kadhaa wanasema walionyesha kufadhaika na wasiwasi wao na familia zao.

Mama yake Shahaf, Ilana, anakumbuka akisema: "Kwa nini tuko hapa ikiwa hakuna mtu anayesikiliza?"

"Aliniambia kuwa wasichana wanaona kuwa kuna fujo. Na nikauliza, 'Je, unalalamika?'

"Na sielewi kabisa jeshi, lakini nilielewa kuwa sio kambi bali ni safu ya juu" ambayo ilihitaji kuchukua hatua, anasema.

Lakini licha ya wasiwasi wa Shahaf, familia yake, kama wengine, walikuwa na imani kamili na jeshi na serikali ya Israeli, na waliamini kwamba hata kama kitu kinapangwa, kingeshughulikiwa haraka.

Shahaf and her mum, pictured smiling and wearing sunglasses on a sunny day
Maelezo ya picha,

Shahaf, upande wa kushoto, akiwa katika picha na mama yake

"Katika miezi iliyopita alisema tena na tena kutakuwa na vita, utaona. Na tulimcheka kwa kutia chumvi," Ilana anakumbuka, akivuta pumzi kubwa kati ya maneno.

Shahaf alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuuawa tarehe 7 Oktoba, wakati Hamas iliposhambulia Nahal Oz.

Ingekuja kuwa siku mbaya zaidi katika historia ya Israeli, ambapo watu 1,300 waliuawa, kulingana na ofisi ya waziri mkuu, na 240 kuchukuliwa mateka.

Mashambulizi ya anga na ardhini yaliyoanzishwa na Israel kujibu mashambulizi hayo yameendelea na kuua zaidi ya watu 23,000 huko Gaza, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas.

Ingawa hawakujua wakati huo, sio tatzpitaniyot pekee waliozua wasiwasi, na uchunguzi wao haukuwa tu habari za kijasusi kwamba kuna kitu kinakuja.

Kwa mujibu wa ripoti katika gazeti la New York Times , mchoro mrefu unaoeleza mipango ya Hamas ulikuwa mikononi mwa maafisa wa Israel kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya tarehe 7 Oktoba, lakini ukatupiliwa mbali kama matamanio tu ya kundi hilo.

Mchambuzi mkongwe katika shirika la kijasusi la Israel Unit 8200 alionya miezi mitatu kabla ya mashambulizi kwamba Hamas ilifanya mazoezi makali ya mafunzo ambayo yalionekana sawa na ilivyoainishwa kwenye ramani, lakini wasiwasi wake ulipuuzwa, gazeti hilo linaripoti.

Mazoezi hayo yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine yenye silaha pia yalikuwa yamechapishwa hadharani kwenye mitandao ya kijamii.

Wanawake 'hawakupata umakinifu ambao walipaswa kupewa'

"Ishara zilikuwa zikibubujika," anasema Meja Jenerali mstaafu Eitan Dangot. "Unapokusanya ishara zote, ungefanya uamuzi wa mapema na kufanya kitu kuizuia.

"Kwa bahati mbaya hili ni jambo ambalo halikufanyika."

Anasema kwamba ingawa uchunguzi kamili bado haujafanywa, ni wazi kwamba ripoti kutoka kwa walinzi "hazikupata umakini wanaopaswa kuwa nazo".

"Wakati mwingine inahusiana na kujiamini kwa maafisa wakuu... 'Sawa, nakusikia, lakini najua bora kuliko wewe. Nina uzoefu. Mimi ni mkubwa kuliko wewe. Nina picha ya kimkakati, na haiwezi kuwa hivyo unachoniambia,' kwa mfano.

"Au wakati mwingine inaweza pia kuwa taasubi za kiume," anasema.

“Kwa ujasusi unatakiwa ukae kwenye meza ya duara na kukusanya taarifa kisha utengeneze fumbo lako, na hawa watu unapotaka kujua nini kinaendelea ni lazima ukae nao kusikiliza kwa makini wanachokuambia wewe, ni nini njia yao ya kuichambua."

Brig Jenerali Amir Avivi, naibu kamanda wa zamani wa kitengo cha Gaza, haamini kuwa ubaguzi wa kijinsia ulikuwa sababu, lakini anakubali kwamba mengi yalipaswa kufanywa kushughulikia wasiwasi wa walinzi.

"Siwezi kusema kwa uhakika kilichotokea lakini naweza kusema kile kinachotarajiwa," anasema.

“Kinachotarajiwa ni kwamba watu wa mipakani wanapofanya kazi zao na wanakuwa na wasiwasi na kuona mambo ambayo yanastahili kuangaliwa na kutathminiwa, mnatakiwa kuwasikiliza kwa sababu wao ndio wataalamu na macho ya kikosi na brigedi na kitengo."

Anasema "Hatua kubwa ya kufeli" ilikuwa "kudhani kwamba wao [Hamas] wamezuiwa" - dhana kwamba "ndiyo wanafanya mazoezi, ndiyo wana mpango lakini hawatautekeleza".

IDF imeahidi uchunguzi , na kujibu maombi ya BBC kwa kusema: "Maswali ya aina hii yataangaliwa baadaye."

Waangalizi wana maoni tofauti kuhusu kwa nini ripoti zao hazikupata jibu kubwa, lakini Avigail anashiriki maoni ya watu kadhaa tuliozungumza nao: "Ni kwa sababu sisi ni askari wa chini zaidi katika mfumo ... kwa hivyo neno letu linachukuliwa kuwa la chini ya kitaaluma."

“Kila mtu alituona kama macho tu, haoni askari,” anasema Roni.

Miezi mitatu baada ya mashambulizi hayo, tatzpitaniyot na familia zinazoomboleza za waliouawa zinatatizika kuafikiana na kile kilichotokea huku wakisubiri uchunguzi.

Katika chumba cha kulala cha Shai Ashram, beti za kijeshi zimetundikwa kwenye meza ya kuvaa, ambayo juu yake kuna michoro na picha zake akiwa amevalia sare.

Baba yake, Dror, anasema wakati mwingine huingia chumbani na kulia.

Shai's father Dror looking pensive as he lights candels
Maelezo ya picha,

Babake Shai Dror anasema anahisi “wivu” anapowaona wanajeshi wengine wakiwa na baba zao

"Alipenda kazi yake sana. Alipenda jeshi na alipenda kuwa mwanajeshi," anasema.

"Mimi ni dereva wa teksi nachukua watu kutoka kituo cha gari moshi na nikiona askari ambaye baba yake anamchukua naumia sana, nina wivu."

Unaweza Pia Kusoma

'Iko nami kila mahali'

Akiwa nyumbani kwa familia yake, Noa hutazama kila siku video za zamani za mitandao ya kijamii za marafiki zake wakiimba na kucheza kambini. Yeye hulala kwenye sofa kila usiku, akiogopa kuwa peke yake katika chumba chake cha kulala.

"Iko pamoja nami kila mahali - katika ndoto na mawazo, kwa kukosa usingizi na kukosa hamu ya kula," anasema. "Mimi sio mtu yule yule niliyekuwa."

Kupitia gumzo la WhatsApp aliloshiriki na wengine wa tatzpitaniyot , ananyooshea majina yao, akisema "wameuawa" au "walitekwa nyara".

Katika kituo chake, Nahal Oz, chumba ambamo tatzpitaniyot ilifanya kazi sasa kimekuwa magofu, na skrini walizotazama wakati Hamas wakijiandaa kwa shambulio lake zimechomwa na kutiwa giza.

Hamas walipopitia Nahal Oz, waliua makumi ya watu.

Miongoni mwa waliokufa ni wengi wa wanawake ambao walitazama mpaka kwa karibu sana kwa ajili ya taifa la Israeli, na ambao walithubutu kuogopa - licha ya kujua uwezo na rasilimali nyingi za Israeli - kwamba kitu kama hiki kinaweza kutokea siku moja.

Taarifa ya ziada ya Idan Ben Ari.

Ubunifu na taswira na Tural Ahmedzade, Matt Thomas, na Gerry Fletcher.

Imehaririwa na Samuel Horti

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah

Soma zaidi
SHARE KWA WENGINE





Comments

UWABATA TV

UWABATA TANGAZO

Kwanini ulaji wa nyama za watu katika nchi za Ulaya ulitumika kama tiba ya hali ya juu?

INSIGNIA LIMITED COMPANY

GRUMETI FUND TRUST,

Total Tanzania Careers 2021, Total Tanzania Jobs 2021

TECHNICIAN II (ELECTRICAL)