Israel yasitisha mapigano mjini Rafah huku wakaazi wakielezea mashambulizi 'yasiyofikirika''
- Get link
- X
- Other Apps
Mjini Gaza Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limetangaza ‘’kusimamishwa kwa shughuli za kijeshi kwa muda’’kwa madhumuni ya kibinadamu" mjini Rafah hadi nane za mchana kwa saa za eneo.
Hatua hii inafuatia usiku wa mashambulizi ya Israeli katika mji wa kusini, ambapo watu wengi kutoka mahali maeneo mbali mbali ya Gaza wamekimbilia.
Samir Qeshta anasema nyumba yake "iliharibiwa kabisa" katika shambulio hilo.
"Nyumba hii ilinihifadhi mimi na watoto wangu. Nilikuwa nikijiandaa kwa ajili ya mwanangu wa kiume kuoa ndani yake, nilikuwa nimeipaka rangi," aliambia shirika la habari la AFP.
"Sisi ni watu wa amani, walitupiga bila tahadhari. Nilikuwa nikimtembelea dada yangu na mke wangu alikuwa nyumbani kwa wazazi wake."
Nimma al-Akhras alikuwa nyumbani wakati mashambulizi ya mabomu yalipoanza.
"Mashambulizi yalikuwa sio ya kufikirika," anasema. “Tulianza kupiga kelele na sikuweza kusogea hadi mtu akanibeba na kuniweka kwenye mkokoteni.
"Tumekosea nini? Tulikuwa tumekaa tu. Si salama majumbani mwetu wala nje, sijui twende wapi?"
Israel inasema inawalenga magaidi na miundombinu yao - na kwamba inajaribu kupunguza vifo vya raia.
Soma zaidi
SHARE kwa wengine
Comments