Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi

Je, ni kweli kuwa Hamas iliundwa na Israel?

 


Madai kwamba vuguvugu la Hamas ulikuwa mradi wa Israel yamekuwa yakisambazwa kwenye vyombo vya habari na wasomi - tangu wapiganaji hao wawaue na kuwateka nyara Waisraeli tarehe 7 Oktoba. Kuna ukweli gani nyuma ya madai hayo?

Wanachama wengi wa Hamas wanakataa madai hayo kama wanavyokataa maafisa wa ngazi za juu wa Israel. Lakini madai hayo yaliwahi kusemwa hadharani na Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak.

Pia, Seneta wa chama cha Republican katika Bunge la Marekani alipata kutoa madai hayo na vilevile yamejadiliwa na maafisa wa usalama wa ndani wa Israel, Shin Bet.

Pia Unaweza Kusoma

Udugu wa Kiislamu

Mapambano ya muda mrefu ya Hamas yana mizizi yake katikati ya miaka ya 1940 katika maeneo ya Wapalestina, wakati matawi ya kwanza ya Muslim Brotherhood yalipoanzishwa huko Gaza, Jerusalem na miji mingine.

Baada ya vita vya Waarabu na Israel vya mwaka 1967, vijana wa Muslim Brotherhood hawakuridhika na viongozi wao wa kidini na kisiasa.

Nyaraka za Muslim Brotherhood (udugu wa kiislamu) zinaonyesha vuguvugu hilo lililenga zaidi kuwa na harakati za kielimu, kitamaduni, kijamii na kiroho, na sio shughuli za kijeshi.

xs

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Muslim Brotherhood ilitokana na mwanazuoni wa Kiislamu Sayyid Qutb, aliyeuwawa Egypt1966

Msemaji wa Hamas

Msemaji wa kwanza wa vuguvugu la Hamas, Ibrahim Ghosheh, anasema katika kitabu chake, The Red Minaret, kulikuwa na maswali mengi miongoni mwa vijana wa chama cha Muslim Brotherhood.

"Kwani haikutoa suluhisho la wazi juu ya mustakabali wa Palestina, na haikutoa wito wa kuanza kwa harakati za wanajihadi wa Kiislamu," anaandika.

Hilo liliwafanya vijana wa Brotherhood - ambao walitaka kupigana na Israeli - kuunda kile kundi lao ndani ya kikundi. Walipanga kujizatiti bila viongozi wa Brotherhood kujua.

j

CHANZO CHA PICHA,GETTYIMAGES

Maelezo ya picha,

Mwishoni mwa miaka ya 1960, vijana kutoka Muslim Brotherhood walifanya mashambulizi dhidi ya Israel chini ya mwanvuli wa Fatah

Makubaliano yalifanywa na vuguvugu la Fatah - lililoongozwa kwa miaka mingi na Yasser Araft - kutoa mafunzo kwa wanachama hao wa Brotherhood.

Uamuzi wa kuzindua Hamas ulikuja baada ya Muslim Brotherhood kupitia changamoto kubwa - ikiwa ni pamoja na kuasi kwa wanachama wengi.

zx

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wafuasi wa Hamas huko Gaza 1992

'Israel iliunda Hamas kukabiliana na PLO'

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak alikuwa miongoni mwa walioibua tuhuma hii. Anasikika katika video akisema mbele ya wanajeshi miongo kadhaa iliyopita, "Israel iliunda Hamas ili kufanya kazi dhidi ya Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO)."

fdc

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kambi ya Fatah huko Jordan, 1970 - Yasser Arafat na wenzake walianzisha vuguvugu la Fatah 1965 kupambanana Israel

Ron Paul, ambaye aligombea urais wa Marekani mwaka 1988, alisema Bungeni mwaka 2009, "ukirejea katika historia, utakuta Israel ilichochea na kusaidia kuunda Hamas, kwa lengo la kukabiliana na Yasser Arafat."

Hassan Asfour, waziri wa zamani na mjumbe wa Palestina katika mazungumzo ya Oslo mwaka 1993, aliiambia televisheni ya BBC mwaka 2023, "Hamas ilizinduliwa kwa makubaliano ya baadhi ya nchi za Kiarabu na Israel - ukiwa ni mradi wa Marekani ili iwe mbadala wa PLO."

pp

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

David Ben-Gurion, mmoja wa waanzilishi wa taifa la Israel akiwa na Mkuu wa Jeshi la srael, Yitzhak Rabin na wanajeshi baada ya ushindi dhidi ya Waarabu 1967

Je, Israel iliifadhili Hamas?

Mwaka 1981, gazeti la New York Times lilichapisha mahojiano na gavana wa kijeshi wa wakati huo wa Israel huko Gaza, Yitzhak Segev, ambaye alisema, "watu wenye imani kali ya Kiislamu wanapokea baadhi ya misaada ya Israel. Serikali ya Israel ilinipa bajeti na serikali ya kijeshi inatoa msaada katika misikiti.”

Alisema: "Fedha hizi zinalenga kuimarisha kikosi kinachoshindana na vuguvugu la Ukombozi wa Palestina (PLO)."

Katika mahojiano yaliyochapishwa hivi karibuni na Shirika la Utangazaji la Israel, Yaakov Perry, afisa wa zamani wa Shin Bet, alisema: “Nilikuwa mkuu wa shirika hilo kuanzia 1988 hadi 1995. Nilishuhudia kuibuka kwa vuguvugu la Hamas, na ninakumbuka tathmini yetu ilikuwa - hili ni kundi la kijamii tu. Likifanya kazi ya kutoa mahitaji kwa watu. Lakini watu wengi Israel waliishutumu Shin Bet kusaidia shughuli za kisiasa za Hamas kama mbadala wa PLO, lakini hilo si kweli."

k

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wanawake wakisoma katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat, Gaza 1970

Mwanzilishi wa Hamas, Sheikh Ahmed Yassiin alisema Israel - ilitoa mishahara ili kujaribu kurejesha maisha ya kawaida kwa watu baada ya kuikalia Gaza.

"Nilikuwa nikipokea lira 240 za Kiisraeli kwa mwezi kwa ajili ya kazi yangu ya ualimu na lira 40 kwa ajili ya kazi yangu kama mhubiri msikitini."

Mtafiti katika Taasisi ya Truman ya Chuo Kikuu cha Hebrew huko Jersulam na afisa wa zamani wa ujasusi wa Israel katika miaka ya 1970, Roni Shaked ameiambia BBC, "Israel haikuwahi kuwafadhili Waislam. Ilitoa leseni kwa taasisi kufanya kazi, lakini haikutoa fedha."

Roni Shaked anasema "hilo linaweza kuwa liliwezesha harakati ya Kiislamu ya Muslim Brotherhood (kabla Hamas kuzaliwa) kukua, lakini Israel haikuwa inaunga mkono harakati zao zisizo na vurugu hapo awali"

kk

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mwanajeshi wa Israel akipiga doria Gaza 1973

Waandishi wa Israel Ehud Yaari na Zeev Schiff wanasema katika kitabu chao cha Intifada cha mwaka 1990, “Israel ilijidanganya kuhusu uwezo wa kuwadhibiti Waislamu wa siasa kali na kuwatumia ili kuudhoofisha ushawishi wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina. Israel imejifunza lakini imechelewa mno.”

jk

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Khan Yunis kusini mwa Gaza 1969

Kupambana na Israel

zx

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Fatah wakizungumza na mpiganaji wa Hamas aliyefunika uso huko Gaza 1993

Mabadiliko makubwa katika mbinu ya mapambano ya Muslim Brotherhood dhidi ya Israel yalitokea mwaka 1983. Katika mkutano wa Jordan, iliamua "kuruhusu wanachama wake katika Ukingo wa Magharibi na Gaza kuandaa harakati za kijeshi," kwa mujibu wa tawasifu ya msemaji wa kwanza wa Hamas, Ibrahim Ghosheh.

Mwaka mmoja baadaye, Israel iliwakamata wanachama wote wa kijeshi huko Gaza, waliokuwa wakiongozwa na Ahmed Yassin na kupata silaha 80 katika nyumba yake.

xs

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wa mbele-kuanzia kulia: Ramadan Shalah (mwanzilishi mwenza wa Islamic Jihad), Ahmed Jibril (wa PLO), Hassan Nasrallah (Kiongozi wa Hezbollah), Khaled Mashal (kiongozi wa Hamas 1996 - 2017) na Sheikh Ahmed Yassin (mwanzilishi wa Hamas)

Lakini Yassin aliachiliwa miezi michache baadaye mwaka 1985 kama sehemu ya makubaliano makubwa ya kuwaachilia wanajeshi watatu wa Israel waliotekwa.

Ahmed Yassin alianza tena jukumu la kuongoza harakati za kijeshi takribani mwaka mmoja baada ya kuachiliwa kwake.

xz

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ahmed Yassin alirudi kuendelea kuongoza wapiganaji wa Kipalestina baada ya mwaka mmoja

Je, Hamas ni zao la Israel yenyewe?

Israel haikuitengeneza Hamas, bali vuguvugu la Muslim Brotherhood na mzozo wa Palestina na Israel ndio sababu kuu ya kuundwa Hamas.

Huenda kukawa na jambo la kujadili iwapo Israel ililifumbia macho vuguvugu hilo wakati wa kuanzishwa kwake, au pengine Israel ilijaribu kuitumia Hamas kwa maslahi yake wakati inachipua na kupata nguvu miongoni mwa Wapalestina.

SOMA ZAIDI


Comments

UWABATA TV

UWABATA TANGAZO

Kwanini ulaji wa nyama za watu katika nchi za Ulaya ulitumika kama tiba ya hali ya juu?

INSIGNIA LIMITED COMPANY

GRUMETI FUND TRUST,

Total Tanzania Careers 2021, Total Tanzania Jobs 2021

TECHNICIAN II (ELECTRICAL)