Mwanamke wa Marekani ahukumiwa miaka 26 kwa mauaji ya mama yake
- Get link
- X
- Other Apps
Mwanamke mmoja nchini Marekani ambaye alisaidia kumuua mama yake na kuuweka mwili wake kwenye sanduku wakati wa likizo ya 2014 huko Bali amehukumiwa kifungo cha miaka 26 jela.
Heather Mack alipatikana na hatia nchini Indonesia mwaka 2015 na kuhukumiwa miaka 10 jela, lakini akaachiliwa huru mwaka wa 2021.
Kisha alikamatwa alipofika Marekani na kushtakiwa kwa njama ya kumuua raia wa Marekani.
Mack amekaa miaka miwili iliyopita katika gereza la Chicago alipokuwa akisubiri hukumu.
Siku ya Jumatano, Jaji Matthew Kennelly aliamua kwamba Mack, 28, atapokea afueni kwa muda ambao amehudumu hadi sasa, na hivyo kupunguza kifungo chake rasmi hadi takriban miaka 23.
Waendesha mashtaka walikuwa wamependekeza kifungo cha miaka 28 jela kwa Mack, ambaye alipanga njama na mpenzi wake wa wakati huo Tommy Schaefer kumuua mamake, msomi tajiri Sheila von Wiese-Mack.
Wawili hao inasemekana walifanya hivyo ili kupata $1.5m (£1.17m) mali iliyowekwa katika hazina ambayo bintiye angeipata baadaye.
Waendesha mashtaka walidai kuwa Bi Mack - ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 wakati wa mauaji hayo na mjamzito - aliziba mdomo wa mamake huku Bw Schaefer akimpiga kichwani kwa bakuli la matunda.Mwili huo baadaye uligunduliwa ukiwa umeingizwa ndani ya sanduku.
Baada ya mauaji ya Wiese-Mack katika hoteli hiyo, Bi Mack na Bw Schaefer waliacha sanduku la mabaki yake kwenye buti ya teksi, waendesha mashtaka walisema.Baadaye dereva alitoa taarifa kwa polisi.
Wanandoa hao waligunduliwa baadaye wakiwa katika hoteli nyingine huko Bali.
Wakati wa hukumu yake, kakake Wiese-Mack, Bill Wiese, aliiomba mahakama kutoa adhabu ya juu iwezekanavyo, akisema kuwa Mack hajaonyesha kujutia uhalifu huo
Soma zaidi
Comments