Mnada wa vitu vya Mandela: Afrika Kusini yataka kuzuia uuzaji juu ya urithi
- Get link
- X
- Other Apps
Serikali ya Afrika Kusini inajaribu kusitisha mnada wenye utata wa vitu 70 vya kibinafsi vya shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela.
Ni pamoja na seti ya vifaa vya usikivu, kitambulisho, zawadi kutoka kwa viongozi wa dunia na baadhi ya mavazi ya rais wa kwanza wa kidemokrasia, kama vile mashati yake ya "Madiba".
Binti yake mkubwa, Makaziwe Mandela, anapiga mnada bidhaa hizo nchini Marekani.
Lakini serikali ya Afrika Kusini inasema bidhaa hizo ni mali ya taifa hilo.
Chini ya sheria ya nchi, vitu vinavyochukuliwa kuwa vya urithi wa kitaifa haviwezi kuchukuliwa nje ya Afrika Kusini.
Wakala wa Rasilimali za Urithi wa Afrika Kusini (Sahra), chombo cha serikali kilichopewa dhamana ya kulinda historia na utamaduni wa nchi hiyo, kilisema kuwa kimewasilisha rufaa ya kuzuia uuzaji huo.
Ombi hilo limeungwa mkono na wizara ya michezo, sanaa na utamaduni. Waziri Zizi Kodwa alisema anaunga mkono kesi hiyo "kwa ajili ya kudumisha urithi tajiri wa nchi".
Aliongeza kuwa kuzuia uuzaji huo ni muhimu kwani Mandela "ni muhimu kwa urithi wa Afrika Kusini".
"Kwa hivyo ni muhimu kwamba tuhifadhi urithi wa Rais wa zamani Mandela na kuhakikisha kwamba uzoefu wa maisha yake wa kazi unabaki nchini kwa vizazi vijavyo."
Serikali ilipinga mnada huo ulipotangazwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2021, ikisema kwamba baadhi ya bidhaa zilizopendekezwa kuuzwa ni za sanaa za kitaifa.
Kama matokeo, mnada wa awali, ambao ulikuwa umepangwa kwa 2022, ulighairiwa na vita vya kisheria vya miaka miwili vikafuata.
Mwezi uliopita, Mahakama Kuu ya Pretoria hatimaye ilimpa Bi Mandela idhini ya kuuza bidhaa hizo, ikipinga hoja ya serikali kwamba ni za urithi wa kitaifa.
SOMA ZAIDI
Comments