Jaribio la Marekani kurejea mwezini katika miaka 50 lagonga mwamba
- Get link
- X
- Other Apps
Chombo cha anga za juu cha Marekani kilichozinduliwa wiki iliyopita kujaribu kutua Mwezini kimesitisha ujumbe wake baada ya kulipuka juu ya Bahari ya Pasifiki.
Chombo hicho kwa jina Peregrine One kilipata hitilafu ambayo iliharibu matarajio yoyote ya kutua kwenye mwezi na kiliamriwa kujiangamiza chenyewe badala yake.
Opereta hiyo ya kibinafsi, Astrobotic yenye makao yake Pittsburgh, ilikielekeza chombo hicho kwenye angahewa ya Dunia ili kuteketea.
Kituo cha ufuatiliaji huko Canberra, Australia, kilithibitisha kupotea kwa rada ya Peregrine saa 20:59 GMT.
Lengo la wanaanga lilikuwa kuwasilisha vifaa vitano kwa Nasa kwenye uso wa Mwezi, ili kuchunguza mazingira ya ndani kabla ya kurudi kwa wanaanga baadaye muongo huu.
Iwapo chombo hicho cha Peregrine kingefanikiwa kutua, ingekuwa misheni ya kwanza ya Marekani katika nusu karne kufanya hivyo, na mradi wa kwanza kabisa wa kibinafsi kufikia mafanikio hayo.
Comments