TANZANIA YASITSHA SAFARI ZA NDEGE ZA SHIRKA LA NDEGE LA KENYA AIRWAYS KATIKA MZOZO MPYA
- Get link
- X
- Other Apps
Mamlaka ya Usafiri
wa Anga nchini Tanzania imetangaza kusitisha safari za ndege za abiria za
Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kuanzia Januari 22, mwaka huu.
Hatua hiyo inakuja
baada ya Mamlaka ya Ndege nchini Kenya kukataa ombi la Shirika la Ndege la
Tanzania (ATCL) kuruhusu ndege ya mizigo ya Air Tanzania kusafirisha mizigo
kutoka Nairobi kwenda mataifa mengine.
Mkurugenzi Mkuu wa
mamlaka hiyo, Hamza Johari ameiambia BBC kuwa, uamuzi wa Tanzania unatokana na
vikwazo vinavyowekwa na mamlaka za Kenya kuzuia shughuli za ndege ya abiria ya
Air Tanzania.
Johari alisema,
“Sababu za kuzuia ndege zao ni za msingi, KQ inakuja kwetu (Tanzania) bila
vikwazo, lakini sisi ndege yetu ya Air Tanzania inawekewa vikwazo kinyume na
Makubaliano yetu ya kibiashara ya huduma za ndege tuliyosaini Novemba mwaka
2016.
Mkurugenzi huyo
aliongeza kuwa wamekuwa wakitafuta mamlaka hiyo ya Kenya kwa ajili ya
usuluhishi bila mafanikio.
“Tumewaandikia
barua hawajibu, pia tumekutana nao bila mafanikio. Lakini kama wakitaka
tubadili uamuzi wetu, basi waje mezani tukubaliane juu ya vikwazo vilivyopo
kwani mpaka sasa tumepata hasara. Mfano kwa safari moja ya ndege ya mizigo
tunapata hasara ya dola za kimarekani 330,000,” alisema Johari.
Mwaka 2020, mamlaka
za Tanzania zilisimamisha safari za KQ kati ya Nairobi na viwanja vya Tanzania
kama Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar kwa kile ilichodai kuwa Kenya
iliiwekea vikwazo mbalimbali vya kibiashara.
SHARE KWA WENGINE
Comments