Kwanini ulaji wa nyama za watu katika nchi za Ulaya ulitumika kama tiba ya hali ya juu?
- Get link
- X
- Other Apps
Ulaya wa nyama za watu katika bara la Ulaya kati ya karne za 14 na 16 ulijulikana kama tiba ya hali ya juu ya maradhi ya kifafa na kupata uungwaji mkono wa hali ya juu kutoka kwa mamlaka za Ulaya.
Matumizi ya "maiti kama dawa " katika kipindi hocho hujulikana kama, The renaissance yanaweza kugawanywa katika makundi mawili.
Tiba iliyokuwa maarufu ilikuwa ikifahamika kama ile ya "mummy", ambapo mgonjwa alilishwa nyama ya binadamu iliyokaushwa, mara kwa mara ikisasafishwa , sawa na kupakwa dawa sawa na maiti za Wamisri.
Lakini baadhi ya madaktari walitumia dawa za kukausha maiti sawa na zile zinazotumiwa nyakati hizi. Hizi ni pamoja na mafuta ya nyama na damu, pamoja na nyama za misuli, zilizotibiwa kwa uangalifu kabla ya kutumiwa. Mamlaka kadhaa zilidai kuwa vyanzo bora vya dawa hiyo ya nyama ya binadamu " vilikuwa ni nyama nyekundu za maiti za wanaume …zisizokuwa na kasoro yoyote…za vijana wenye umri wa karibu miaka 24, asiye na kasoro yoyote " na ambaye aliuawa kwa " kifo cha ukatili ".
Matayarisho mengine yalikuwa ni pamoja na fuvu la binadamu, pamoja na "usnea", au spishi ambaye huota kwenye fuvu la kichwa cha binadamu baada ya kufa.
Tiba ya kundi la "Mummy" ilitumiwa hususan kutibu magonjwa ya kutokwa na damu au kidonda cha mwili.
Damu iliyochanganywa na fuvu kwa pamoja vilikaushwa na kusagwa kama unga ambao ulitumiwa kutibu ugonjwa wa kifafa.
Ulaji wa nyama ya watu
Kwa sababu ambazo hazijafahamika wazi, matumizi ya maiti za watu kama dawa hayajaorodheshwa miongoni mwa dawa zilizotumiwa katika historia ya dawa za binadamu .Hatahivyo, tiba ya aina hiyo ilitokana na imani za kishirikina au udanganyifu uliotumia njama.
Mtindo huu ambao chimbuko lake ni dawa ya kitamaduni ya Waarabu, ulipendekezwa au kukubaliwa na wasomi wengi, wakiwemo wanafarsafa walioishi kabla ya sayansi ikiwa ni pamoja na Francis Bacon; mshairi na mhubiri John Donne; na mkemia Robert Boyle.
Mwaka 1685, matone yaliyotoka kwenye fuvu la binadamu yalikuwa miongoni mwa tiba zilizotolewa kwa Mfalme King Charles II ambaye alikuwa anakufa.
Ni wazi kuwa, dawa ya maiti ilikuwa ni aina ya ulaji wa nyama za watu.
Tangu mwishoni mwa karne ya kumi na tano kuendelea, watu wa Ulaya na karibu dunia nzima walilaani "ulaji wa nyama za watu " Marekani hivi karibuni iligundua ,hatahivyo kuwa hakuna yeyote aliyeelezea matumizi ya tiba hii kama ulaji wa nyama za maiti za watu.
"Dawa nzuri"
Ni kwa vipi tiba hizi ziliendelea kushamiri kwa muda mrefu licha ya kuwa katika tamaduni zilizoiona kama jambo la kutisha?
Mamlaka za matibabu zilikuwa na usiri mkubwa , ikiwa ni pamoja na matumizi ya lugha ya Kilatini pamoja udhibiti wa wachache wa mfumo wa tiba hii "halali" yalikuwa ni mambo muhimu katika kuficha tiba ya ulaji wa nyama za binadamu.
Wakati fulani kabla ya mwaka 1599, msafiri mmoja alirekodi kile alichokiona katika piramidi katika mji mkuu wa Misri nchini Cairo: alisema kwamba, " miili ya watu wa kale ilikuwa inafufuliwa kila siku, wala sio miili iliyooza , "na " hawa maiti …ambao madaktari walikuwa wanatulazimisha tuwameze kinyume na utashi wetu''.
Kauli hii inaonesha kuwa madaktari walikuwa na mamlaka ya kuwalazimisha wagonjwa wa kifafa kunywa mchanganyiko wa majimaji ya vipande vya nyama za wafu waliokaushwa (mummy)
Mnamo mwaka 1647, Mhubiri na muandishi Thomas Fuller alielezea wafu waliokaushwa kama '' dawa nzuri lakini chakula kibaya " ." Kauli yake inaonesha kwamba dawa hii kwa kiasi fulani ilichanganywa na nyama ya binadamu mbichi, jambo linalothihirisha kuwa kweli ulikuwa ni ulaji wa nyama za binadamu.
Hatahivyo, mchakato wa matibabu haya haukutegemea nguvu ya ''sayansi'', bali ulitegemea dini au imani za kichawi au imani kuhusu nguvu za kiroho za mwili wa binadamu.
Nguvu ya maisha ya kiroho
Katika karne ya 14 hadi ya 15, ambacho kilikuwa ni kipindi cha mabadiliko ya kihistoria barani Ulaya , roho ya binadamu ilihusika katika mchakato wa kimsingi wa kisaikolojia wa binadamu.
Katika nadharia, roho yenyewe haikuwa na maana. Lakini ilikuwa inaminiwa kuwa ilikuwa ndani ya mwili na ilikuwa pamoja na roho nyingine zenye nguvu, zilizoundwa kwa mchanganyiko wa damu na hewa.
"Roho" hawa waliaminiwa kuzunguka ndani ya viumbe na waliaminiwa kuwa walikuwa kila mahali kwa wakati mmoja, ikimaanisha kuwa ulikuwa ni mchakato wa kisaikolojia.
Roho hawa waliaminiwa kuwa ndio kiini cha uhai wa binadamu, kiunganishi muhimu ambacho kiliunganisha Mungu na maisha ya kawaida ya kidunia.
Kwa mawazo ya watu walioishi kipindi cha zama za kati, dawa ya kula nyama ya mfu ilikuwa ni kitu ambacho kilitoa fursa ya mtu kupata maisha ya kiroho.
Kwa mawazo yao walipoifikiria damu ya binadamu, walidhani kuwa mgonjwa alipokunywa au kula nyama ya mfu alipata moja kwa moja maisha halisi kwasababu vilitoka kwenye mwili uliokuwa hai kabla ya kufa.
Katika miaka ya mwisho ya karne ya kumi na saba, waziri wa kanisa la kale la Kiprotestanti Edward Taylor alisema " damu ya binadamu, ya moto na baridi, ni ya manufaa dhidi ya magonjwa."
Katika mwaka 1747, madaktari Waingereza bado walikuwa wanawashauri watu kunywa kile walichokiita " damu ya moto " ya binadamu kama tiba ya ugonjwa wa kifafa.
Dawa ya roho
Dawa ya miili ya maiti za watu huenda ilimaanisha mambo tofauti kwa watu tofauti.
Kwa baadhi, huenda ilikuwa ikitumika kwa imani kwamba ingeweza kurekebisha athari za biashara, bidhaa, lakini kwa wengine ilionekana kama kiunganishi cha binadamu na utakatifu zaidi wa binadamu.
Sources BBC SWAHILI
Comments