Posts

Showing posts from January, 2024

Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi

UNRWA ni nini na kwa nini ufadhili wake umesimamishwa?

Image
  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Umoja wa Mataifa hutoa huduma muhimu Gaza kama vile maji wakati miundombinu ikiwa karibu kushindwa kufany akazi baada ya zaidi ya siku 100 za mashambulizi ya anga ya Israel Saa 8 zilizopita Na Aine Gallagher BBC Global Digital Wakati nchi za Magharibi zikisitisha ufadhili kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, baada ya madai ya Israel kwamba wafanyakazi wake wachache walishiriki katika shambulio la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, tunaangalia kile UNRWA inafanya na jinsi inavyofadhiliwa. UNRWA ni nini? UNRWA inasimama kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Usaidizi na Kazi kwa Wakimbizi wa Palestina katika eneo la karibu la Mashariki . Inaendesha shule, huduma za kijamii, vituo vya afya na kusambaza misaada ya chakula kwa wakimbizi wa Palestina milioni 5.9 mjini Gaza, Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel, pamoja na Lebanon, Syria na Jordan. Ilianzishwa wakati gani? Ilianzishwa mwaka 1949 kwa ajili y

Wasiwasi waibuka huku M23 ikiunda utawala mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Image
  Kundi la waasi la M23 limeteua utawala wake katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na hivyo kuzua wasiwasi Katika taarifa ya kundi hilo, kiongozi wa kisiasa wa M23 Bertrand Bisimwa amesema kundi hilo limeteua watawala katika eneo la Rutshuru la Kivu Kaskazini. Aliongeza kuwa viongozi wa miji ya Kiwanja, Rubare na Bunagana, katika Kivu Kaskazini, wameteuliwa pia. Waasi wanadhibiti sehemu kubwa ya Rutshuru na Masisi, mbili kati ya wilaya tano zinazounda jimbo la Kivu Kaskazini, na ziko takriban kilomita 35 (maili 22) magharibi mwa mji mkuu wa mkoa huo, Goma. Katika siku za hivi karibuni, jeshi la Congo limeanzisha mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani katika maeneo yanayodhibitiwa na M23. Siku ya Jumatano msemaji wa kundi hilo alisema wapiganaji wake waliiangusha moja ya ndege zisizo na rubani tatu zilizokuwa zikitumiwa na jeshi. BBC haijathibitisha dai hili kwa duru huru, wala jeshi halijatoa maoni kulihusu. Mitandao ya kij

Mnada wa vitu vya Mandela: Afrika Kusini yataka kuzuia uuzaji juu ya urithi

Image
  Serikali ya Afrika Kusini inajaribu kusitisha mnada wenye utata wa vitu 70 vya kibinafsi vya shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela. Ni pamoja na seti ya vifaa vya usikivu, kitambulisho, zawadi kutoka kwa viongozi wa dunia na baadhi ya mavazi ya rais wa kwanza wa kidemokrasia, kama vile mashati yake ya "Madiba". Binti yake mkubwa, Makaziwe Mandela, anapiga mnada bidhaa hizo nchini Marekani. Lakini serikali ya Afrika Kusini inasema bidhaa hizo ni mali ya taifa hilo. Chini ya sheria ya nchi, vitu vinavyochukuliwa kuwa vya urithi wa kitaifa haviwezi kuchukuliwa nje ya Afrika Kusini. Wakala wa Rasilimali za Urithi wa Afrika Kusini (Sahra), chombo cha serikali kilichopewa dhamana ya kulinda historia na utamaduni wa nchi hiyo, kilisema kuwa kimewasilisha rufaa ya kuzuia uuzaji huo. Ombi hilo limeungwa mkono na wizara ya michezo, sanaa na utamaduni. Waziri Zizi Kodwa alisema anaunga mkono kesi hiyo "kwa ajili ya kudumisha urithi tajiri wa nchi". Aliongeza kuwa

Je, ni kweli kuwa Hamas iliundwa na Israel?

Image
  Madai kwamba vuguvugu la Hamas ulikuwa mradi wa Israel yamekuwa yakisambazwa kwenye vyombo vya habari na wasomi - tangu wapiganaji hao wawaue na kuwateka nyara Waisraeli tarehe 7 Oktoba. Kuna ukweli gani nyuma ya madai hayo? Wanachama wengi wa Hamas wanakataa madai hayo kama wanavyokataa maafisa wa ngazi za juu wa Israel. Lakini madai hayo yaliwahi kusemwa hadharani na Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak. Pia, Seneta wa chama cha Republican katika Bunge la Marekani alipata kutoa madai hayo na vilevile yamejadiliwa na maafisa wa usalama wa ndani wa Israel, Shin Bet. Pia Unaweza Kusoma Uharibifu wa maeneo ya kidini huko Gaza 17 Januari 2024 Walikuwa macho ya Israeli kwenye mpaka - lakini tahadhari zao kuhusu Hamas hazikusikika 15 Januari 2024 Maafisa wa Israel wanataka kuiangamiza Gaza- Mahakama ya ICJ yafahamishwa 11 Januari 2024 Udugu wa Kiislamu Mapambano ya muda mrefu ya Hamas yana mizizi yake katikati ya miaka ya 1940 katika maeneo ya Wapalestina, wakati matawi ya kwanza ya Mus