Trump aitaka Iran kuingia makubaliano ya nyuklia, akionya kuhusu mashambulizi ya kikatili zaidi

  Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Iran kufanya makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia, akisema aliipa Tehran nafasi baada ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kuhusu makubaliano yalikuwa yanakaribia kuingia awamu ya sita Jumapili. "Niliwaambia, kwa maneno makali, "fanyeni tu," ingawa walijaribu sana, haijalishi walikuwa karibu vipi, hawakuweza kufanikiwa," Trump anaandika kwenye mtandao wa kijamii wa Truth. "Iran lazima ifanye makubaliano na kuokoa kile ambacho hapo awali kilijulikana kama Dola ya Iran. Hakuna kifo tena, hakuna uharibifu tena, FANYA TU, KABLA HAMJACHELEWA." Hapo awali Trump alisema anafahamu mipango ya Israel kabla ya kuanza mashambulizi usiku kucha, lakini aliweka wazi kuwa wanajeshi wa Marekani hawakushiriki katika operesheni hiyo.

Wanajeshi watatu wa Marekani wauawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani Mashariki ya Kati




Wanajeshi watatu wa Marekani wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye kituo cha Marekani karibu na mpaka wa Jordan na Syria.

Rais wa Marekani Joe Biden alisema shambulio hilo lilitekelezwa na "makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali wanaoungwa mkono na Iran". Aliongeza: "Tutajibu."

Ni mara ya kwanza kwa shambulio kuua wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo tangu shambulio la Hamas la tarehe 7 Oktoba dhidi ya Israel.

Jordan inasema shambulio hilo lilifanyika Syria, sio ndani ya Jordan.

Kumekuwa na mashambulizi mengine kwenye kambi za Marekani katika eneo hilo lakini hadi sasa hakuna majeraha walioripotiwa na jeshi la Marekani.

Haijabainika ni nani aliyetekeleza shambulio hili la hivi punde.

Rais Biden alisema Marekani "itawawajibisha wale wote wanaohusika kwa wakati na kwa njia tunayochagua".
S0MA ZAIDI HAPA

Comments

UWABATA TV

UWABATA TANGAZO

INSIGNIA LIMITED COMPANY

Kwanini ulaji wa nyama za watu katika nchi za Ulaya ulitumika kama tiba ya hali ya juu?

GRUMETI FUND TRUST,

Total Tanzania Careers 2021, Total Tanzania Jobs 2021

TECHNICIAN II (ELECTRICAL)