Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi

“Ndoa ya wazazi wangu ilizua kashfa ya kimataifa”

 

g

CHANZO CHA PICHA,PERSONAL ARCHIVES

Maelezo ya picha,

Uamuzi wa Muingereza Ruth Holloway na Mkenya John Kimuyu kuoana uligonga vichwa vya habari

Na,Jeremy Mpira

BBC News, Nottingham (Uingereza)

Ilikuwa ni hadithi nyingine ya mapenzi, lakini uhusiano wa kimapenzi kati ya mmishonari Mzungu Mwingereza Ruth Holloway na mhudumu wa simu mweusi Mkenya John Kimuyu uligeuka kuwa kashfa kubwa kwenye vyombo vya habari mwishoni mwa miaka ya 1950.

Baada ya vifo vyao, hivi karibuni, binti yao Ndinda Kimuyu alianza kuandika kitabu kuhusu hadithi ya wazazi wake.

John, ambaye alikuwa na ulemavu wa macho, alikutana na Ruth katika Taasisi ya Wasioona ya Kenya ambako alifanyia kazi.

Ruth alikuwa na umri wa miaka 19 tu alipoondoka kwenda Kenya, baada ya kukulia katika mji mdogo wa Kirkby-in-Ashfield, Nottinghamshire, Uingereza.

f
Maelezo ya picha,

Ndinda Kimuyu anaandika kitabu kuhusu hadithi ya mapenzi ya wazazi wake.

Ndinda anasema wakati wanandoa hao walipoamua kufunga ndoa, mama yake alipanda boti kurejea Uingereza kuwajulisha wazazi na mabosi wake juu ya uamuzi huo, lakini hawakukubali.

"Lilikuwa tatizo kubwa sana," Bi Ndinda aliiambia BBC. "Wakati wa safari hii, Jeshi la Wokovu liliamua kuchukua kazi yake."

"Aliishia kununua pete ya harusi, akatengeneza keki na pete ya ndoa ndani na kuisafirisha kwa magendo hadi Kenya."

Wenzi hao walipendana wakati wa hali ya wasi wasi katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Jeshi la Kenya la Ardhi na Uhuru, linalojulikana kama Mau Mau, lilipigania uhuru dhidi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza.

w

CHANZO CHA PICHA,PERSONAL ARCHIVES

Maelezo ya picha,

Gazeti moja linatangaza "ndoa ya siri na Mwafrika asiyeona".

Muungano wa wanandoa hao ulikuwa na utata hasa kwa sababu Ruth aliaminika kuwa Mzungu wa kwanza kuolewa na Mkenya mweusi.

Sherehe hiyo ilikatishwa hata na msajili - ambaye aliwafungisha ndoa , lakini akasema hakubaliani na ndoa hiyo.

Ndinda anasema harusi hiyo iliripotiwa kwenye magazeti na televisheni nchini Uingereza, Kenya, Marekani na kwingineko.

Baadhi ya ripoti zilionyesha kuwa ndoa hiyo ilitishia kusababisha machafuko ya rangi.

f

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ndoa hiyo iliambatana na ghasia zilizopelekea Kenya kupata uhuru na kuzidisha suala la ubaguzi wa rangi.

"Pengine upinzani mkali ulitoka kwa wakoloni weupe nchini Kenya," anakumbuka binti huyo, aliyezaliwa miaka mitatu baada ya ndoa.

"Mama yangu hangeweza kushinda, wala baba yangu. Kulikuwa na makala chache chanya, lakini kwa ujumla zilikuwa za ubaguzi wa rangi."

"Ndoa ya wazazi wangu ya rangi tofauti ilisababisha kashfa ya kimataifa."

Familia hiyo ilianza kutengana baada ya Kenya kupata uhuru mwaka wa 1963, kwa kuwa walihofia maisha ya Ruth kwani nchi hiyo mpya ilikuwa "imewataka wazungu wote kuondoka".

Mnamo 1965, wanandoa waliamua kwamba Ruth amrudishe Ndinda na dada zake wawili Uingereza.

"Nilikasirika sana," Ndinda anakumbuka. "Tulifika na sanduku letu dogo na nguo zetu na tumekuwa hapa tangu wakati huo."

"Ulikuwa wakati mgumu sana kwa baba yangu. Nadhani [mama yangu] alikuwa na mshtuko wa neva, lakini aliweza kumudu kuishi nao."

Ndinda anasema wazazi wake walidhani kipofu hatapata kazi Uingereza. Kwa hiyo John alibaki Kenya, ambako alifanya kazi kama mhudumu wa simu wa polisi.

g
Maelezo ya picha,

John Kimuyu alituma rekodi ili kuwasiliana na mkewe na binti zake.

Aliendelea kuwasiliana na familia kwa kumtumia Ruth rekodi ambazo Ndinda bado anazihifadhi hadi leo.

Anasema mama yake alijaribu kuwa na matumaini, lakini kutoweza kuwa na mumewe "kuliuvunja moyo wake."

Ruth alifariki takriban miaka 30 iliyopita na John, ambaye alioa tena mara mbili, alifikisha umri wa miaka 90 kabla ya kufariki Novemba mwaka huu.

Ndinda alirejea Kenya kuhudhuria mazishi ya baba yake mwezi uliopita, ikiwa ni safari yake ya kwanza nchini humo baada ya miaka 30.

Safari hii katika nchi yake ya asili ilimtia moyo kuandika kitabu kuhusu hadithi ya wazazi wake.

“Nilihisi niko nyumbani,” anasema. "Sikuwa na huzuni kwa sababu baba yangu alikuwa amefariki. Kwa kweli, nilihisi amani."

"Nilitoka kwenye veranda na kusikia sauti ya mama yangu ikisema waziwazi 'yote ni sawa katika nafsi yangu.'

Ndinda anasema wazazi wake walikuwa "waanzilishi" ambao walisaidia kubadilisha historia.

"Tunaishi katika ulimwengu tofauti leo, lakini ndivyo upendo ulivyo. [Kwa mapenzi, utafanya chochote. Utapanda milima. Ni upendo uliowaleta pamoja na ndio upendo uliowaruhusu kupigania haya yote. .”

Comments

UWABATA TV

UWABATA TANGAZO

Kwanini ulaji wa nyama za watu katika nchi za Ulaya ulitumika kama tiba ya hali ya juu?

INSIGNIA LIMITED COMPANY

GRUMETI FUND TRUST,

Total Tanzania Careers 2021, Total Tanzania Jobs 2021

TECHNICIAN II (ELECTRICAL)