Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi

Je, Iran inapanga nini juu ya mashambulizi ya Marekani dhidi ya wapiganaji wake nchini Syria, Iraq na Yemen?


.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Iran imethibitisha kuwa haitaki kuingia katika vita dhidi ya Marekani, lakini imeahidi kujibu kwa nguvu mashambulizi yoyote dhidi ya ardhi yake au dhidi ya maslahi yake katika Mashariki ya Kati.

Rais wa Iran Ebrahim Raisi ndiye aliyekuwa mhusika wa hivi punde zaidi wa Iran kusisitiza ujumbe huu: "Hatutapigana vita yoyote, lakini kama kuna nchi, mvamizi au nduli anayetaka kutudhulumu, tutakuwa thabiti katika kujibu hilo."

Kauli ya rais wa Iran imekuja baada ya Marekani kushambulia maeneo yanayolengwa na Iran nchini Syria na Iraq kugonga vichwa vya habari - ikiwa ni sehemu ya jibu la Washington kwa shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye kambi ndogo ya kijeshi ya Marekani inayojulikana kwa jina la "Burj 22" huko Jordan karibu na mpaka wa Iraq.

Shambulio hilo lilisababisha vifo vya wanajeshi watatu wa Marekani na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, ikiwa ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Marekani kuuawa huku kukiwa na machafuko makubwa ya kikanda yaliyosababishwa na shambulio la Oktoba 7 lililotekelezwa na Hamas katika maeneo ya Israel na kuongezeka kwa jeshi la Israel la kushambulia kwenye Ukanda wa Gaza.

Rais wa Marekani Joe Biden alisema kwamba wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran ndio waliohusika na shambulio hilo kwenye kambi ya Marekani, na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin pia alithibitisha kwamba ndege iliohusika na mashambulizi hayo ilitoka Iran.

Ameongeza kuwa wanamgambo hao wamelenga vituo na vikosi vya kijeshi vya Marekani angalau mara 160 tangu tarehe 7 Oktoba. Hata hivyo, waziri wa Marekani alionyesha kwamba mashambulizi mengi hayakuwa na ufanisi kabisa.

Iran inakanusha wakati wote kwamba inahusika na mashambulizi haya ya wapiganaji, na kusisitiza kwamba makundi yenye silaha hayapokei amri zao kutoka Tehran.

Austin alisema mashambulizi ya Marekani yatafanyika katika viwango tofauti, na kwamba yanaweza kuendelea kwa siku kadhaa, yakilenga maslahi ya Iran na makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na Tehran nchini Iraq na Syria.

Lakini nia kuu ya Washington ni kuepuka kufanya jambo lolote litakalopelekea kuongezeka kwa vita katika eneo hilo. Utawala wa Marekani uko chini ya shinikizo kutoka kwa Warepublican kuilenga Iran yenyewe, na kupendekeza kuwa jibu kali dhidi ya Iran litapunguza uwezekano wa mashambulizi dhidi ya maslahi ya Marekani.

Lakini utawala wa Biden uliamua kuepuka kulenga shabaha katika ardhi ya Iran, jambo ambalo limetuma ujumbe kwa Tehran kwamba haitaki mambo yakose udhibiti.

Bado haijabainika iwapo Iran inajiandaa kwa mashambulizi, lakini ripoti zimeibuka hivi karibuni zikionyesha kwamba Tehran imeita vikosi vyake vingi kutoka katika eneo hilo.

Kumekuwa na visa huko nyuma ambapo Iran na Marekani zilijulishana kabla ya mashambulizi ili kuepusha majeruhi.

Lakini Kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Iran Hossein Salami aliionya Marekani akisema, “Mmetujaribu kwenye uwanja wa vita na tumekujaribuni pia. Hatutaacha tishio lolote bila kuchukua hatua za kukabiliana na hali hiyo, na ingawa hatutafuti vita, hatuogopi wala kuvikimbia.”

Inaonekana kuwa Iran inajaribu kupunguza makali ya hali kwa njia nyinginezo, kama kamanda wa Kikosi cha Quds, chenye mafungamano na Iran.

.

CHANZO CHA PICHA,AFP

Maelezo ya picha,

Mpaka wa Jordan na Syria

Qaani aliwataka wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Iraq kupunguza mashambulizi yao, jambo ambalo lilisababisha kundi muhimu lenye silaha miongoni mwao kukubali kusitisha operesheni zao.

Wanamgambo wa "Hezbollah Brigades" wa Iraq, wanaoshukiwa kutekeleza shambulio la Jumapili iliyopita kwenye kambi ya Marekani, walitangaza kwamba wataacha kulenga vikosi vya Marekani kwa ombi la Iran.

Hata hivyo, makundi mengine yenye silaha yalitangaza wazi kwamba yataendeleza mashambulizi yao yenye lengo la kuwatimua wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo.

Kauli hizi zinaonyesha kuwa Iran inaweza isiwe na udhibiti kamili juu ya makundi haya licha ya kuyafadhili na kuyapa silaha, lakini hii haionekani kuathiri hesabu za Marekani, kama Waziri wa Ulinzi Austin alivyosema: "Siku zote tunasikiliza kile watu wanasema na pia kufuatilia wanachofanya.”

Ni wazi kuwa Iran ina nia ya kutojiingiza katika vita vikubwa zaidi vya kieneo katika eneo hilo, lakini ikiwa itategemea ni mambo gani yanaweza kutokea, itakuwa vigumu kwake kujiepusha na ongezeko hilo.

Uamuzi kuhusu jibu la Iran umetolewa na Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ambaye anaweka na kusimamia sera za Iran katika Mashariki ya Kati kupitia Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran.

Khamenei amekaa kimya kuhusu suala hili hadi sasa. Pia anajua vyema kwamba hakuna usawa kati ya Iran na Marekani, lakini pia anajua kuwa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi kinaweza kusababisha matatizo mengi katika eneo.

Comments

UWABATA TV

UWABATA TANGAZO

Kwanini ulaji wa nyama za watu katika nchi za Ulaya ulitumika kama tiba ya hali ya juu?

INSIGNIA LIMITED COMPANY

GRUMETI FUND TRUST,

Total Tanzania Careers 2021, Total Tanzania Jobs 2021

TECHNICIAN II (ELECTRICAL)