Mpalestina aliyeshinda tuzo ya Grammy ashambuliwa na walowezi wa Israel na kukamatwa na jeshi
.jpg)
Rais wa Marekani Donald Trump amesema atazidisha ushuru kwenye chuma na alumini bidhaa zinazotoka Canada kutoka asilimia 25% hadi asilimia 50%.
Katika vita vya kibiashara vinavyoendelea, Trump amesema hatua hii ni kulipiza kisasi kwa ushuru wa asilimia 25 ambao Ontario iliweka kwa umeme inayoupeleka kwa majimbo ya kaskazini ya Marekani.
Akijibu tangazo la Trump, waziri mkuu wa Ontario amesema “hatutajinyenyekea” na kumtaka Trump “aache fitina”.
Trump amesema ushuru huu utaanza Jumatano, na kuongeza kwamba atatangaza hali ya “dharura ya kitaifa kuhusu umeme” katika majimbo hayo.
Hatua hii inajiri baada ya siku mbaya zaidi ya mwaka 2025 kwa masoko ya Marekani, yaliyosababishwa na hofu ya ushuru mkali wa Rais Donald Trump dhidi ya washirika wake wakubwa wa kibiashara.
Alipohojiwa kuhusu uwezekano wa kudorora kwa uchumi wa Marekani, Trump alisema uchumi uko katika “kipindi cha mabadiliko.”
Comments