Posts

Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi

Je, Iran inapanga nini juu ya mashambulizi ya Marekani dhidi ya wapiganaji wake nchini Syria, Iraq na Yemen?

Image
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Saa 1 iliyopita Iran imethibitisha kuwa haitaki kuingia katika vita dhidi ya Marekani, lakini imeahidi kujibu kwa nguvu mashambulizi yoyote dhidi ya ardhi yake au dhidi ya maslahi yake katika Mashariki ya Kati. Rais wa Iran Ebrahim Raisi ndiye aliyekuwa mhusika wa hivi punde zaidi wa Iran kusisitiza ujumbe huu: "Hatutapigana vita yoyote, lakini kama kuna nchi, mvamizi au nduli anayetaka kutudhulumu, tutakuwa thabiti katika kujibu hilo." Kauli ya rais wa Iran imekuja baada ya Marekani kushambulia maeneo yanayolengwa na Iran nchini Syria na Iraq kugonga vichwa vya habari - ikiwa ni sehemu ya jibu la Washington kwa shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye kambi ndogo ya kijeshi ya Marekani inayojulikana kwa jina la "Burj 22" huko Jordan karibu na mpaka wa Iraq. Shambulio hilo lilisababisha vifo vya wanajeshi watatu wa Marekani na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, ikiwa ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Marekani kuuawa huku kukiwa na macha

Wanajeshi watatu wa Marekani wauawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani Mashariki ya Kati

Image
Getty Images Copyright: Getty Images Wanajeshi watatu wa Marekani wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye kituo cha Marekani karibu na mpaka wa Jordan na Syria. Rais wa Marekani Joe Biden alisema shambulio hilo lilitekelezwa na "makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali wanaoungwa mkono na Iran". Aliongeza: "Tutajibu." Ni mara ya kwanza kwa shambulio kuua wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo tangu shambulio la Hamas la tarehe 7 Oktoba dhidi ya Israel. Jordan inasema shambulio hilo lilifanyika Syria, sio ndani ya Jordan. Kumekuwa na mashambulizi mengine kwenye kambi za Marekani katika eneo hilo lakini hadi sasa hakuna majeraha walioripotiwa na jeshi la Marekani. Haijabainika ni nani aliyetekeleza shambulio hili la hivi punde. Rais Biden alisema Marekani "itawawajibisha wale wote wanaohusika kwa wakati na kwa njia tunayochagua". S0MA ZAIDI HAPA

Marekani yaidhinisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa Iran nchini Syria na Iraq

Image
Getty Images Copyright: Getty Images Wanajeshi wa Marekani Image caption: Wanajeshi wa Marekani Marekani imeidhinisha mipango ya mfululizo wa mashambulizi dhidi ya malengo ya Iran nchini Syria na Iraq, maafisa wameiambia mshirika wa BBC Marekani CBS News. Mashambuliizi hayo yatafanyika kwa siku kadhaa, maafisa wanasema, na hali ya hewa huenda itaamuru ini lini yatazinduliwa. Hatua hiyo inajiri baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani kuwaua wanajeshi watatu wa Marekani huko Jordan, karibu na mpaka wa Syria, siku ya Jumapili.Marekani imelilaumu kundi la wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran kwa shambulio hilo. Kundi la Islamic Resistance in Iraq - ambalo linaaminika kuwa na wanamgambo wengi ambao wamejihami, kufadhiliwa na kupewa mafunzo na kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran - limesema ndilo lililohusika na shambulio hilo. Iran imekanusha kuhusika na shambulio hilo lililojeruhi wanajeshi wengine 41 wa Marekani katika kambi ya kijeshi. Wakati maafisa wa Marekani wameahidi kujibu ma

“Ndoa ya wazazi wangu ilizua kashfa ya kimataifa”

Image
  CHANZO CHA PICHA, PERSONAL ARCHIVES Maelezo ya picha, Uamuzi wa Muingereza Ruth Holloway na Mkenya John Kimuyu kuoana uligonga vichwa vya habari Saa 4 zilizopita Na,Jeremy Mpira BBC News, Nottingham (Uingereza) Ilikuwa ni hadithi nyingine ya mapenzi, lakini uhusiano wa kimapenzi kati ya mmishonari Mzungu Mwingereza Ruth Holloway na mhudumu wa simu mweusi Mkenya John Kimuyu uligeuka kuwa kashfa kubwa kwenye vyombo vya habari mwishoni mwa miaka ya 1950. Baada ya vifo vyao, hivi karibuni, binti yao Ndinda Kimuyu alianza kuandika kitabu kuhusu hadithi ya wazazi wake. John, ambaye alikuwa na ulemavu wa macho, alikutana na Ruth katika Taasisi ya Wasioona ya Kenya ambako alifanyia kazi. Ruth alikuwa na umri wa miaka 19 tu alipoondoka kwenda Kenya, baada ya kukulia katika mji mdogo wa Kirkby-in-Ashfield, Nottinghamshire, Uingereza. Maelezo ya picha, Ndinda Kimuyu anaandika kitabu kuhusu hadithi ya mapenzi ya wazazi wake. Ndinda anasema wakati wanandoa hao walipoamua kufunga ndoa, mama yake a

UNRWA ni nini na kwa nini ufadhili wake umesimamishwa?

Image
  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Umoja wa Mataifa hutoa huduma muhimu Gaza kama vile maji wakati miundombinu ikiwa karibu kushindwa kufany akazi baada ya zaidi ya siku 100 za mashambulizi ya anga ya Israel Saa 8 zilizopita Na Aine Gallagher BBC Global Digital Wakati nchi za Magharibi zikisitisha ufadhili kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, baada ya madai ya Israel kwamba wafanyakazi wake wachache walishiriki katika shambulio la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, tunaangalia kile UNRWA inafanya na jinsi inavyofadhiliwa. UNRWA ni nini? UNRWA inasimama kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Usaidizi na Kazi kwa Wakimbizi wa Palestina katika eneo la karibu la Mashariki . Inaendesha shule, huduma za kijamii, vituo vya afya na kusambaza misaada ya chakula kwa wakimbizi wa Palestina milioni 5.9 mjini Gaza, Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel, pamoja na Lebanon, Syria na Jordan. Ilianzishwa wakati gani? Ilianzishwa mwaka 1949 kwa ajili y