Tundu Lissu afikishwa Mahakamani asomewa shitaka la uhaini

 


Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini tanzania, Chadema, Tundu Lissu jioni hii amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka moja la uhaini.

Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la Wakili Nassoro Katuga

Awali Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilisema lilimkamata Lissu jana mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025.

Aidha Polisi nchini humo kupitia taarifa yake ilitoa onyo kwa vyama vyote vya siasa kutotoa maneno ya uchochezi, kashfa kwa Polisi na Serikali au viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Mapema Polisi walipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema huku wakizua viongozi wa chama hicho kufanya mkutano na waandishi wa habari.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kushikiliwa pia kwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, John Heche, Mjumbe wa Kamati kuu, Godbless Lema, Mwenyekliti wa chama hecho kanda ya Kusini, Aden Mayala na Mkurugenzi wa Mawasiliano na uenezi, Brenda Rupia.


Lissu alikamatwa hapo jana baada ya kumaliza mkutano wa hadhara mkoani Ruvuma, kusini mwa Tanzania. Akiendelea kunadi msimamo wa chama hicho wa 'No Reforms, No Election,

No Reforms, No Election, ni msimamo wa kisera wa chama hicho uliopitishwa na Kamati Kuu katika kikao chake cha Disemba 2-3, 2024 unaodai kuwa CHADEMA haitoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu kama hakutafanyika mabadiliko ya kimfumo katika uchaguzi, ikiwa ni pamoja na marekebisho ya katiba, sheria, na kuhakikisha kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi.

Zaidi Lissu na chama hicho unaeleza kwamba uchaguzi hautafanyika nchini humo kama marekebisho wanayodai hayatafanyika.

Taarifa ya jana ya chama hicho inadai kutofanyiwa haki na jeshi hilo.

SOURCE BBC SWAHILI


Comments

UWABATA TV

UWABATA TANGAZO

Kwanini ulaji wa nyama za watu katika nchi za Ulaya ulitumika kama tiba ya hali ya juu?

INSIGNIA LIMITED COMPANY

GRUMETI FUND TRUST,

Total Tanzania Careers 2021, Total Tanzania Jobs 2021

TECHNICIAN II (ELECTRICAL)