Tundu Lissu afikishwa Mahakamani asomewa shitaka la uhaini
.jpg)
TikTok haipatikani mtandaoni nchini Marekani, saa chache kabla ya sheria mpya ya kupiga marufuku jukwaa hilo kuanza kutumika.
Ujumbe ulioonekana kwenye programu kwa watumiaji wa Marekani ulisema sheria ya kupiga marufuku TikTok imepitishwa, kumaanisha "huwezi kutumia TikTok kwa sasa".
"Tuna bahati kwamba Rais Trump amedokeza kuwa atashirikiana nasi kutafuta suluhisho la kurejesha TikTok mara tu atakapoingia madarakani," ilisomeka.
Hili linawadia baada ya mtandao huo wa kijamii kuonya kwamba huduma zake "zitapotea" siku ya Jumapili isipokuwa kama utawala unaoondoka wa Biden utatoa hakikisho kwamba marufuku hiyo haitatekelezwa.
Rais mteule Donald Trump amesema "uwezekano mkubwa zaidi" ni kwamba ataipa TikTok siku 90 ili kuepuka marufuku hiyo mara tu atakapoingia madarakani Jumatatu.
Watumiaji waliripoti kuwa programu hiyo pia ilikuwa imeondolewa kwenye Apple na Google ya Marekani huku TikTok.com haikuwa inaonyesha video.
"Kuongeza muda wa siku 90 ni jambo ambalo kuna uwezekano mkubwa litatekelezwa, kwa sababu ndio hatua sahihi kuchukuliwa," Trump aliambia NBC News siku ya Jumamosi.
"Nikiamua kufanya hivyo, kuna uwezekano nikatangaza Jumatatu."
Ikulu ya White House ilisema ni jukumu la utawala unaokuja kuchukua hatua.
"Hatuoni sababu ya TikTok au kampuni zingine kuchukua hatua katika siku chache zijazo kabla ya utawala wa Trump kuchukua madaraka Jumatatu," katibu wa waandishi wa habari Karine Jean-Pierre alisema katika taarifa.
Comments