Posts

Showing posts from 2025

Tundu Lissu afikishwa Mahakamani asomewa shitaka la uhaini

Image
  Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini tanzania, Chadema, Tundu Lissu jioni hii amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka moja la uhaini. Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la Wakili Nassoro Katuga Awali Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilisema lilimkamata Lissu jana mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025. Aidha Polisi nchini humo kupitia taarifa yake ilitoa onyo kwa vyama vyote vya siasa kutotoa maneno ya uchochezi, kashfa kwa Polisi na Serikali au viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mapema Polisi walipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema huku wakizua viongozi wa chama hicho kufanya mkutano na waandishi wa habari. Vyombo vy...

Mpalestina aliyeshinda tuzo ya Grammy ashambuliwa na walowezi wa Israel na kukamatwa na jeshi

Image
 Mshindi wa tuzo ya Oscar ya Palestina ameshambuliwa na walowezi wa Israel, wanaharakati walioshuhudia tukio hilo wanasema, kabla ya kukamatwa na jeshi la Israel. Hamdan Ballal, mmoja wa wakurugenzi wenza wanne wa shirika la ‘No Other Land{hakuna Ardhi Nyingine} , alikuwa na nyumba yake katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel ikiwa imezingirwa na walowezi wakati wa shambulio la Jumatatu, Kituo cha Kundi la Waasi wa Kiyahudi (CJNV) kilisema. Mkurugenzi mwenza Yuval Abraham alisema Bw Ballal alipigwa na walowezi kisha kuchukuliwa na wanajeshi akiwa kwenye gari la wagonjwa. Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema hakuna Mpalestina aliyezuiliwa kutoka kwa gari la wagonjwa. Bila kumtaja Bw Ballal, IDF ilisema Wapalestina watatu na Muisraeli wamezuiliwa kwa tuhuma za "kurusha mawe" kwa vikosi vya usalama. Mwanaharakati ambaye alikuwa katika eneo la tukio aliambia BBC kuwa Wapalestina watatu waliozuiliwa, akiwemo Bw Ballal, walijeruhiwa katika shambulio la walowezi na sasa ...

Tshisekedi na Kagame wakutana na kukubaliana kusitisha vita DRC

Image
  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame walikutana nchini Qatar Jumanne hii kwa mazungumzo yao ya kwanza ya ana kwa ana tangu waasi wa M23 waanze mashambulizi mashariki mwa Kongo mwezi Januari, taarifa ya pamoja ya serikali tatu ilisema. Mkutano huo uliosimamiwa na Amir wa Qatar, unakuja siku moja baada ya kundi la M23 kujitoa kwenye mazungumzo mengine ya Angola, ikiwa tayari imeteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Kongo. Kongo inaishutumu Rwanda kwa kutuma silaha na wanajeshi wa Rwanda kuwaunga mkono waasi hao, ambao mashambulizi yao yameitumbukiza mashariki mwa Kongo katika mzozo wake mbaya zaidi katika miongo kadhaa. Rwanda imesema kuwa vikosi vyake vinafanya kazi ya kujilinda dhidi ya jeshi la Kongo na wanamgambo wanaoishambulia Kigali., ikikana kuiunga mkono M23.

Trump atangaza ushuru zaidi kwa alumini na chuma kutoka Canada

  Rais wa Marekani Donald Trump amesema atazidisha ushuru kwenye chuma na alumini bidhaa zinazotoka Canada kutoka asilimia 25% hadi asilimia 50%. Katika vita vya kibiashara vinavyoendelea, Trump amesema hatua hii ni kulipiza kisasi kwa ushuru wa asilimia 25 ambao Ontario iliweka kwa umeme inayoupeleka kwa majimbo ya kaskazini ya Marekani. Akijibu tangazo la Trump, waziri mkuu wa Ontario amesema “hatutajinyenyekea” na kumtaka Trump “aache fitina”. Trump amesema ushuru huu utaanza Jumatano, na kuongeza kwamba atatangaza hali ya “dharura ya kitaifa kuhusu umeme” katika majimbo hayo. Hatua hii inajiri baada ya siku mbaya zaidi ya mwaka 2025 kwa masoko ya Marekani, yaliyosababishwa na hofu ya ushuru mkali wa Rais Donald Trump dhidi ya washirika wake wakubwa wa kibiashara. Alipohojiwa kuhusu uwezekano wa kudorora kwa uchumi wa Marekani, Trump alisema uchumi uko katika “kipindi cha mabadiliko.” source

TikTok yasitisha huduma zake Marekani saa chache kabla ya kupigwa marufuku

Image
  TikTok haipatikani mtandaoni nchini Marekani, saa chache kabla ya sheria mpya ya kupiga marufuku jukwaa hilo kuanza kutumika. Ujumbe ulioonekana kwenye programu kwa watumiaji wa Marekani ulisema sheria ya kupiga marufuku TikTok imepitishwa, kumaanisha "huwezi kutumia TikTok kwa sasa". "Tuna bahati kwamba Rais Trump amedokeza kuwa atashirikiana nasi kutafuta suluhisho la kurejesha TikTok mara tu atakapoingia madarakani," ilisomeka. Hili linawadia baada ya mtandao huo wa kijamii kuonya kwamba huduma zake "zitapotea" siku ya Jumapili isipokuwa kama utawala unaoondoka wa Biden utatoa hakikisho kwamba marufuku hiyo haitatekelezwa. Rais mteule Donald Trump amesema "uwezekano mkubwa zaidi" ni kwamba ataipa TikTok siku 90 ili kuepuka marufuku hiyo mara tu atakapoingia madarakani Jumatatu. Watumiaji waliripoti kuwa programu hiyo pia ilikuwa imeondolewa kwenye Apple na Google ya Marekani huku TikTok.com haikuwa inaonyesha video. "Kuongeza muda wa si...