Posts

Showing posts from February, 2024

Mpalestina aliyeshinda tuzo ya Grammy ashambuliwa na walowezi wa Israel na kukamatwa na jeshi

Image
 Mshindi wa tuzo ya Oscar ya Palestina ameshambuliwa na walowezi wa Israel, wanaharakati walioshuhudia tukio hilo wanasema, kabla ya kukamatwa na jeshi la Israel. Hamdan Ballal, mmoja wa wakurugenzi wenza wanne wa shirika la ‘No Other Land{hakuna Ardhi Nyingine} , alikuwa na nyumba yake katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel ikiwa imezingirwa na walowezi wakati wa shambulio la Jumatatu, Kituo cha Kundi la Waasi wa Kiyahudi (CJNV) kilisema. Mkurugenzi mwenza Yuval Abraham alisema Bw Ballal alipigwa na walowezi kisha kuchukuliwa na wanajeshi akiwa kwenye gari la wagonjwa. Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema hakuna Mpalestina aliyezuiliwa kutoka kwa gari la wagonjwa. Bila kumtaja Bw Ballal, IDF ilisema Wapalestina watatu na Muisraeli wamezuiliwa kwa tuhuma za "kurusha mawe" kwa vikosi vya usalama. Mwanaharakati ambaye alikuwa katika eneo la tukio aliambia BBC kuwa Wapalestina watatu waliozuiliwa, akiwemo Bw Ballal, walijeruhiwa katika shambulio la walowezi na sasa ...

Urusi inatengeneza silaha mpya ya kushambulia satelaiti - Marekani

Image
  CHANZO CHA PICHA, EPA Maelezo ya picha, Wataalamu waliambia BBC kwamba silaha yoyote inaweza kusababisha machafuko kwa tegemeo la setilaiti ya Marekani (picha ya faili) 16 Februari 2024 Urusi inatengeneza silaha mpya ya kupambana na satelaiti, Marekani imesema, lakini ilisisitiza kuwa Moscow bado haijaitumia. Msemaji wa Ikulu ya Marekani John Kirby alitoa maoni hayo siku moja baada ya mjumbe mkuu wa chama cha Republican kutoa onyo lisilo wazi la "tishio kubwa la usalama wa taifa". Silaha hiyo ni ya anga za juu na ina silaha ya nyuklia kulenga satelaiti, mshirika wa BBC wa Marekani CBS News aliripoti. Lakini Bw Kirby hakuthibitisha hili na alikataa kutoa maelezo sahihi kuhusu tishio hilo siku ya Alhamisi. Moscow iliishutumu Marekani kwa kutumia madai ya silaha mpya za Kirusi kama mbinu ya kulazimisha Bunge la Congress kupitisha msaada wa ziada wa Ukraine kwa "kivyovyote vile ". Bw Kirby, ambaye hivi majuzi alifanywa msaidizi mkuu wa Rais Joe Biden, aliwaambia waand...

Edward Lowassa afariki dunia

Image
  Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa amefariki dunia, akiwa anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam. Tangazo la kifo cha Lowassa kimetangazwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango. Katika tangazo fupi alilolitoa kupitia televisheni ya taifa, Mpango amesema kuwa Lowassa amefikwa na umauti katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Lowassa alihudumu kama Waziri Mkuu wa Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa miaka mitatu, toka 2005 mpaka 2008 alipolazimika kujiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia hii leo. Mwaka 2015 Lowassa alikihama chama tawala cha CCM baada ya kukosa tiketi ya kuwania urais kupitia chama hicho. Alitimkia chama kikuu cha upinzani cha Chadema ambapo aliungwa mkono kugombea urais na vyama vilivyounda umoja wa upinzani wa UKAWA kwa wakati huo. Lowassa hata hivyo alishindwa katika uchaguzi huo na aliyekuwa mgombea wa C...

Netanyahu akataa mapendekezo ya Hamas ya kusitisha mapigano Gaza

Image
CHANZO CHA PICHA, SERIKALI YA ISRAEL Saa 6 zilizopita Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa mapendekezo ya Hamas ya kusitisha mapigano - akisema "ushindi kamili" huko Gaza unawezekana ndani ya miezi kadhaa. Alikuwa akizungumza baada ya Hamas kuweka msururu wa matakwa kujibu pendekezo la kusitisha mapigano lililoungwa mkono na Israel. Bw Netanyahu alisema mazungumzo na kundi hilo "hayaendi popote" na akaelezea masharti yao kama "ya kustaajabisha". Mazungumzo yanaendelea kujaribu kufikia makubaliano ya aina fulani. "Hakuna suluhu lingine ila ushindi kamili na wa mwisho," Bw Netanyahu aliambia mkutano wa wanahabari Jumatano. "Ikiwa Hamas itasalia Gaza, ni suala la muda tu hadi mauaji yajayo." Israel ilitazamiwa kukabiliana na pendekezo la Hamas, lakini jibu hili ni kama kukemea, na maafisa wa Israel wanaona wazi juhudi za Hamas kumaliza vita kwa masharti yake kama jambo lisilokubalika kabisa. Afisa mkuu wa Hamas Sami Abu Zuhri ...

Kwa nini ubongo wa Lenin ulikatwa vipande zaidi ya 30,000?

Image
  CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Ubongo wa Lenin ulitolewa na madaktari waliomfanyia uchunguzi baada ya kifo chake. Dakika 18 zilizopita Na Juan Francisco Alonso BBC Mundo Baada ya mwanzilishi wa Muungano wa Kisovieti, Vladimir Ilyich Ulyanov, anayejulikana zaidi kama Lenin, kufa mnamo Januari 1924, baadhi ya madaktari waliomtibu walipendekeza kuondoa ubongo wake ili 'kuufanyia utafiti. Miaka mia moja iliyopita, lengo la wanasayansi hawa na washirika wao wa kisiasa lilikuwa ni kugundua uwezo mkubwa wa kiakili ambao ulitambuliwa kama ‘’uwezo mkubwa wa kiakili’’ wa Lenin. Wazo hilo liliidhinishwa na uongozi wa Usoviet, ambao uliunda taasisi ya kufanya utafiti huu. Karne moja baadaye, ubongo wa Lenin uko wapi na ni matokeo gani ya uchambuzi? Ili kujibu maswali haya na mengine, BBC News Mundo, idhaa ya BBC ya Kihispania, ilizungumza na wanahistoria na madaktari wa upasuaji wa neva ambao wamechunguza kisa hicho. CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Daktari ...