Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi

Israel yasema ushahidi unaonyesha mlipuko wa hospitali ulitoka Gaza huku Netanyahu akianza mazungumzo na Biden

 




Rais wa Marekani Joe Biden amemwambia waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba "inaonekana" "shambulio la hospitali ya Al Ahli lilitekelezwa na kundi jingine ".

Biden anasema "amehuzunishwa sana na kukasirishwa" na tukio hilo.

"Kulingana na kile nimeona inaonekana kana kwamba shambulio hilo lilitekelezwa na kundi jingi, sio wewe. Lakini kuna watu wengi huko nje ambao hawana uhakika, kwa hivyo lazima tukabiliane na mambo mengi," alisema.

BBC inajaribu kuunganisha vipande vidogo vidogo vya mlipuko wa hospitali ya jana usiku - ambao Hamas na mamlaka ya Palestina wanailaumu Israel kwa kutekeleza shambulio la angani.

Rais Biden anasema alitembelea Israel ili kuonyesha mahali Marekani iinaunga mkono katika mzozo huo.

Anaendelea kuelezea mauaji ya Hamas tarehe 7 Oktoba. Anasema "siyo sifa " kusema "walichinja" watu 1,300, ikiwa ni pamoja na Wamarekani 31.

Pia alizungumzia kuhusu mateka wa Israeli, pamoja na watoto.

"Hebu fikiria watoto hao waliokuwa wanajificha kutoka kwa Hamas walikuwa wanafikiria nini? Ni zaidi ya ufahamu wangu.

"Marekani itaendelea kuiunga mkono Israel, anasema, akimwambia Netanyahu: "Ninatazamia kuwa na mjadala kuhusu kile kinachotokea hapa.

"Anasema "ujasiri, kujitolea na ushujaa" wa watu wa Israeli "ni wa kustaajabisha", akiongeza "Najivunia kuwa hapa".

Comments

UWABATA TV

UWABATA TANGAZO

Kwanini ulaji wa nyama za watu katika nchi za Ulaya ulitumika kama tiba ya hali ya juu?

INSIGNIA LIMITED COMPANY

GRUMETI FUND TRUST,

Total Tanzania Careers 2021, Total Tanzania Jobs 2021

TECHNICIAN II (ELECTRICAL)