Tundu Lissu afikishwa Mahakamani asomewa shitaka la uhaini

Image
  Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini tanzania, Chadema, Tundu Lissu jioni hii amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka moja la uhaini. Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la Wakili Nassoro Katuga Awali Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilisema lilimkamata Lissu jana mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025. Aidha Polisi nchini humo kupitia taarifa yake ilitoa onyo kwa vyama vyote vya siasa kutotoa maneno ya uchochezi, kashfa kwa Polisi na Serikali au viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mapema Polisi walipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema huku wakizua viongozi wa chama hicho kufanya mkutano na waandishi wa habari. Vyombo vy...

DP WORLD NI NINI

 DP World ni kampuni ya kimataifa ya Emirati inayojihusisha na usafirishaji iliyoko Dubai, Falme za Kiarabu. Imejikita na usafirishaji wa mizigo, shughuli za bandari, huduma za baharini na maeneo ya biashara huria. Iliundwa mwaka 2005 kwa muunganiko wa mamlaka ya bandari ya Dubai (Dubai Ports Authority) na mamlaka ya bandari ya Dubai kimataifa (Dubai Ports International), DP World inashughulikia makontena milioni 70 ambayo huletwa na karibu meli 70,000 kila mwaka. Hii ni sawa na takriban 10% ya makontena yanayosafirishwa ya kimataifa yanayotolewa na vituo vyao 82 vya baharini na nchi kavu vilivyopo katika zaidi ya nchi 40. Hadi mwaka 2016, DP World ndiyo kampuni iliyokuwa ikiendesha bandari kimataifa, na tangu wakati huo, imepata na kushirikiana na makampuni mengine juu na chini ya mnyororo wa thamani.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Zamani[hariri | hariri chanzo]

Dubai Ports International (DPI) ilianzishwa mwaka 1999[1] Mradi wake wa kwanza ulikuwa huko JeddahSaudi Arabia, akishirikiana na mshirika wa ndani kwenye South Container Terminal (SCT). DPI kisha iliendelea na kuendeleza shughuli katika bandari za Djibouti mwaka wa 2000VizagIndia mwaka 2002 na Constanta, Romania mwaka 2003[1] Mnamo Januari 2005, DPI ilipata vituo duniani vya CSX (CSX WT). [2] Baadaye Septemba 2005 ndipo Dubai Ports International iliunganishwa rasmi na mamlaka ya bandari ya Dubai kuunda DP World. [3] Upanuzi wa haraka kupitia ununuzi uliendelea Machi 2006 wakati DP World ilinunua kampuni ya nne kubwa zaidi ya waendeshaji bandari duniani, P&O kwa £3.9 bilioni.

2006: Mzozo wa usalama wa bandari ya Marekani[hariri | hariri chanzo]

Umiliki wa aina mbalimbali za bandari Marekani na DP World ( kama sehemu ya mkataba wa P&O) ilionekana kuwa yenye utata na wengi nchini Marekani ingawa iliungwa mkono na Rais wa Marekani George W. Bush ; bandari za Marekani ziliuzwa muda mfupi baadaye.

P&O iliendesha kampuni kuu za Marekani New YorkNew JerseyPhiladelphiaBaltimoreNew Orleans, na Miami . Kabla ya makubaliano hayo kupatikana, mpango huo ulipitiwa upya na Kamati ya Uwekezaji wa Kigeni nchini Marekani inayoongozwa na Idara ya hazina ya Marekani na zikiwemo Idara za nchi, biashara na Usalama wa Taifa . Ilipewa mwanga wa kijani ilikuendelea na shughuli zake, lakini muda mfupi baadaye, wanachama wote wa Democratic na Republican wa Congress walionyesha wasiwasi juu ya athari mbaya ambayo mpango huo ungekuwa nayo kwa usalama wa bandari.

Source Wikipedia Swahili

Comments

UWABATA TV

UWABATA TANGAZO

Kwanini ulaji wa nyama za watu katika nchi za Ulaya ulitumika kama tiba ya hali ya juu?

INSIGNIA LIMITED COMPANY

GRUMETI FUND TRUST,

Total Tanzania Careers 2021, Total Tanzania Jobs 2021

TECHNICIAN II (ELECTRICAL)