Posts

Tundu Lissu afikishwa Mahakamani asomewa shitaka la uhaini

Image
  Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini tanzania, Chadema, Tundu Lissu jioni hii amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka moja la uhaini. Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la Wakili Nassoro Katuga Awali Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilisema lilimkamata Lissu jana mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025. Aidha Polisi nchini humo kupitia taarifa yake ilitoa onyo kwa vyama vyote vya siasa kutotoa maneno ya uchochezi, kashfa kwa Polisi na Serikali au viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mapema Polisi walipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema huku wakizua viongozi wa chama hicho kufanya mkutano na waandishi wa habari. Vyombo vy...

Jaribio la Marekani kurejea mwezini katika miaka 50 lagonga mwamba

Image
  Chombo cha anga za juu cha Marekani kilichozinduliwa wiki iliyopita kujaribu kutua Mwezini kimesitisha ujumbe wake baada ya kulipuka juu ya Bahari ya Pasifiki. Chombo hicho kwa jina Peregrine One kilipata hitilafu ambayo iliharibu matarajio yoyote ya kutua kwenye mwezi na kiliamriwa kujiangamiza chenyewe badala yake. Opereta hiyo ya kibinafsi, Astrobotic yenye makao yake Pittsburgh, ilikielekeza chombo hicho kwenye angahewa ya Dunia ili kuteketea. Kituo cha ufuatiliaji huko Canberra, Australia, kilithibitisha kupotea kwa rada ya Peregrine saa 20:59 GMT. Lengo la wanaanga lilikuwa kuwasilisha vifaa vitano kwa Nasa kwenye uso wa Mwezi, ili kuchunguza mazingira ya ndani kabla ya kurudi kwa wanaanga baadaye muongo huu. Iwapo chombo hicho cha Peregrine kingefanikiwa kutua, ingekuwa misheni ya kwanza ya Marekani katika nusu karne kufanya hivyo, na mradi wa kwanza kabisa wa kibinafsi kufikia mafanikio hayo. Article share tools Sambaza Tazama njia zaidi za kusambaza Share this post Copy ...

Mwanamke wa Marekani ahukumiwa miaka 26 kwa mauaji ya mama yake

Image
  Mwanamke mmoja nchini Marekani ambaye alisaidia kumuua mama yake na kuuweka mwili wake kwenye sanduku wakati wa likizo ya 2014 huko Bali amehukumiwa kifungo cha miaka 26 jela. Heather Mack alipatikana na hatia nchini Indonesia mwaka 2015 na kuhukumiwa miaka 10 jela, lakini akaachiliwa huru mwaka wa 2021. Kisha alikamatwa alipofika Marekani na kushtakiwa kwa njama ya kumuua raia wa Marekani. Mack amekaa miaka miwili iliyopita katika gereza la Chicago alipokuwa akisubiri hukumu. Siku ya Jumatano, Jaji Matthew Kennelly aliamua kwamba Mack, 28, atapokea afueni kwa muda ambao amehudumu hadi sasa, na hivyo kupunguza kifungo chake rasmi hadi takriban miaka 23. Waendesha mashtaka walikuwa wamependekeza kifungo cha miaka 28 jela kwa Mack, ambaye alipanga njama na mpenzi wake wa wakati huo Tommy Schaefer kumuua mamake, msomi tajiri Sheila von Wiese-Mack. Wawili hao inasemekana walifanya hivyo ili kupata $1.5m (£1.17m) mali iliyowekwa katika hazina ambayo bintiye angeipata baadaye. Waendesh...

TANZANIA YASITSHA SAFARI ZA NDEGE ZA SHIRKA LA NDEGE LA KENYA AIRWAYS KATIKA MZOZO MPYA

Image
 Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania imetangaza kusitisha safari za ndege za abiria za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kuanzia Januari 22, mwaka huu. Hatua hiyo inakuja baada ya Mamlaka ya Ndege nchini Kenya kukataa ombi la Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuruhusu ndege ya mizigo ya Air Tanzania kusafirisha mizigo kutoka Nairobi kwenda mataifa mengine. Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Hamza Johari ameiambia BBC kuwa, uamuzi wa Tanzania unatokana na vikwazo vinavyowekwa na mamlaka za Kenya kuzuia shughuli za ndege ya abiria ya Air Tanzania. Johari alisema, “Sababu za kuzuia ndege zao ni za msingi, KQ inakuja kwetu (Tanzania) bila vikwazo, lakini sisi ndege yetu ya Air Tanzania inawekewa vikwazo kinyume na Makubaliano yetu ya kibiashara ya huduma za ndege tuliyosaini Novemba mwaka 2016. Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wamekuwa wakitafuta mamlaka hiyo ya Kenya kwa ajili ya usuluhishi bila mafanikio. “Tumewaandikia barua hawajibu, pia tumekutana nao bila mafanikio. L...

Walikuwa macho ya Israeli kwenye mpaka - lakini tahadhari zao kuhusu Hamas hazikusikika

Image
  Maelezo kuhusu taarifa Author, Alice Cuddy Nafasi, BBC News, Israel 15 Januari 2024, 06:59 EAT Imeboreshwa Saa 8 zilizopita Wanajulikana kama macho ya Israeli kwenye mpaka wa Gaza . Kwa miaka mingi, vitengo vya vijana wa kike walioandikishwa kujiunga na jeshi vilikuwa na kazi moja hapa. Ilikuwa ni kukaa katika vituo vya uchunguzi kwa saa nyingi, kutafuta dalili za kitu chochote cha kutiliwa shaka. Katika miezi kabla ya mashambulizi ya 7 Oktoba ya Hamas, walianza kuona mambo: mazoezi ya kufanya uvamizi, utekaji nyara , na wakulima kuwa na tabia ya ajabu katika upande mwingine wa ua. Noa, sio jina lake halisi, anasema wangepitisha habari kuhusu kile walichokuwa wakikiona kwa maafisa wa ujasusi na wa ngazi za juu, lakini hawakuwa na uwezo wa kufanya zaidi. "Tulikuwa macho tu," anasema. Ilikuwa wazi kwa baadhi ya wanawake hawa kwamba Hamas ilikuwa inapanga jambo kubwa - kwamba kulikuwa na, kwa maneno ya Noa, "puto ambalo lingepasuka". BBC sasa imezungumza na wasichana...