Posts

Trump aitaka Iran kuingia makubaliano ya nyuklia, akionya kuhusu mashambulizi ya kikatili zaidi

  Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Iran kufanya makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia, akisema aliipa Tehran nafasi baada ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kuhusu makubaliano yalikuwa yanakaribia kuingia awamu ya sita Jumapili. "Niliwaambia, kwa maneno makali, "fanyeni tu," ingawa walijaribu sana, haijalishi walikuwa karibu vipi, hawakuweza kufanikiwa," Trump anaandika kwenye mtandao wa kijamii wa Truth. "Iran lazima ifanye makubaliano na kuokoa kile ambacho hapo awali kilijulikana kama Dola ya Iran. Hakuna kifo tena, hakuna uharibifu tena, FANYA TU, KABLA HAMJACHELEWA." Hapo awali Trump alisema anafahamu mipango ya Israel kabla ya kuanza mashambulizi usiku kucha, lakini aliweka wazi kuwa wanajeshi wa Marekani hawakushiriki katika operesheni hiyo.

Vita vya Ukraine: Marekani yatuma kwa siri makombora ya masafa marefu kusaidia Kyiv

Image
  CHANZO CHA PICHA, REUTERS Ukraine imeanza kutumia makombora ya masafa marefu yaliyotolewa kwa siri na Marekani dhidi ya Urusi, maafisa wa Marekani wamethibitisha. Silaha hizo zilikuwa sehemu ya msaada wa $300m (£240m) ulioidhinishwa na Rais wa Marekani Joe Biden mwezi Machi na ziliwasili mwezi huu. Tayari zimetumika angalau mara moja kulenga shabaha za Urusi katika eneo linalokaliwa la Crimea, ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinasema. Bwana Biden sasa ametia saini kifurushi kipya cha msaada cha $61bn kwa Ukraine. Hapo awali Marekani iliipatia Ukraine toleo la masafa ya kati la Mifumo ya silaha za Makombora (ATACMS) lakini ilikuwa ikisita kutuma kitu chochote chenye nguvu zaidi, kwa sababu ya wasiwasi wa kuhatarisha utayari wa kijeshi wa Marekani. Hata hivyo, Bw Biden anasemekana kuidhinisha kwa siri kutuma mfumo wa masafa marefu - ambao unaweza kurusha makombora umbali wa hadi 300km (maili 186) - mnamo Februari. "Naweza kuthibitisha kwamba Marekani iliipatia Ukraine ATA...

Kwa nini Jordan ilikosolewa baada ya mashambulizi ya anga ya Iran dhidi ya Israel?

Image
CHANZO CHA PICHA, REUTERS 18 Aprili 2024 Uamuzi wa Jordan wa kuunganisha nguvu na Marekani, Uingereza na Ufaransa kuzuia ndege zisizo na rubani na makombora yaliyorushwa na Iran dhidi ya Israel usiku wa Aprili 13 ulikabiliwa na hisia kali ndani ya nchi na eneo hilo. Baada ya kauli za vitisho ya Tehran, Amman alimuita balozi wa Iran siku ya Jumapili. Shirika la habari la Fars liliripoti kwamba vikosi vya jeshi la Iran "vilikuwa vinafuatilia kwa makini mienendo ya Jordan wakati wa mashambulizi ya kuadhibu dhidi ya utawala wa Kizayuni" na kuonya kwamba Jordan itakuwa "shabaha inayofuata" ikiwa itaingilia kati. Jordan, ambayo inapakana na Israel, ndiyo nchi inayohifadhi idadi kubwa zaidi ya Wapalestina na kihistoria imekuwa ikionekana kuwa mfuasi wao mkubwa katika eneo hilo. Mfalme Abdullah, kiongozi wa nchi hiyo ambaye ana mtazamo wa kukosoa vita vya Gaza, aliunga mkono waziwazi juhudi za kupeleka misaada katika eneo hilo kwa njia ya anga. CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGE...

Urusi inatengeneza silaha mpya ya kushambulia satelaiti - Marekani

Image
  CHANZO CHA PICHA, EPA Maelezo ya picha, Wataalamu waliambia BBC kwamba silaha yoyote inaweza kusababisha machafuko kwa tegemeo la setilaiti ya Marekani (picha ya faili) 16 Februari 2024 Urusi inatengeneza silaha mpya ya kupambana na satelaiti, Marekani imesema, lakini ilisisitiza kuwa Moscow bado haijaitumia. Msemaji wa Ikulu ya Marekani John Kirby alitoa maoni hayo siku moja baada ya mjumbe mkuu wa chama cha Republican kutoa onyo lisilo wazi la "tishio kubwa la usalama wa taifa". Silaha hiyo ni ya anga za juu na ina silaha ya nyuklia kulenga satelaiti, mshirika wa BBC wa Marekani CBS News aliripoti. Lakini Bw Kirby hakuthibitisha hili na alikataa kutoa maelezo sahihi kuhusu tishio hilo siku ya Alhamisi. Moscow iliishutumu Marekani kwa kutumia madai ya silaha mpya za Kirusi kama mbinu ya kulazimisha Bunge la Congress kupitisha msaada wa ziada wa Ukraine kwa "kivyovyote vile ". Bw Kirby, ambaye hivi majuzi alifanywa msaidizi mkuu wa Rais Joe Biden, aliwaambia waand...