Trump apotosha kwa kutumia picha ya Congo na kudai ni ya mauaji ya kimbari ya Wazungu wa Afrika Kusini

Rais wa Marekani Donald Trump alionyesha picha iliyochukuliwa katika video ya shirika la habari la Reuters katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kuiwasilisha kama ushahidi wa mauaji ya halaiki ya Wazungu wa Afrika Kusini. "Hawa wote ni wakulima wa kizungu ambao wanazikwa," Trump alisema siku ya Jumatano, akionesha picha hiyo wakati wa mkutano katika Ikulu ya Marekani na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa. Picha hiyo ilitokana na video iliyochapishwa na Reuters Februari 3, 2025, inaonyesha wafanyakazi wa kibinadamu wakinyanyua mifuko yenye miili katika mji wa Goma nchini Congo. Picha hiyo ilitolewa kutoka katika video ya Reuters iliyopigwa kufuatia mapigano makali na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda. Picha hiyo iliyooneshwa na Trump lilichapishwa na American Thinker, jarida la kihafidhina la mtandaoni – likionesha migogoro na mivutano ya kirangi Afrika Kusini na Congo. Ikulu ya White House haikujibu maswali ya Reuters kuhusu picha hiyo. Andrea Widburg, mhariri ...