Posts

Showing posts from 2023

Mpalestina aliyeshinda tuzo ya Grammy ashambuliwa na walowezi wa Israel na kukamatwa na jeshi

Image
 Mshindi wa tuzo ya Oscar ya Palestina ameshambuliwa na walowezi wa Israel, wanaharakati walioshuhudia tukio hilo wanasema, kabla ya kukamatwa na jeshi la Israel. Hamdan Ballal, mmoja wa wakurugenzi wenza wanne wa shirika la ‘No Other Land{hakuna Ardhi Nyingine} , alikuwa na nyumba yake katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel ikiwa imezingirwa na walowezi wakati wa shambulio la Jumatatu, Kituo cha Kundi la Waasi wa Kiyahudi (CJNV) kilisema. Mkurugenzi mwenza Yuval Abraham alisema Bw Ballal alipigwa na walowezi kisha kuchukuliwa na wanajeshi akiwa kwenye gari la wagonjwa. Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema hakuna Mpalestina aliyezuiliwa kutoka kwa gari la wagonjwa. Bila kumtaja Bw Ballal, IDF ilisema Wapalestina watatu na Muisraeli wamezuiliwa kwa tuhuma za "kurusha mawe" kwa vikosi vya usalama. Mwanaharakati ambaye alikuwa katika eneo la tukio aliambia BBC kuwa Wapalestina watatu waliozuiliwa, akiwemo Bw Ballal, walijeruhiwa katika shambulio la walowezi na sasa ...

Israel yasema ushahidi unaonyesha mlipuko wa hospitali ulitoka Gaza huku Netanyahu akianza mazungumzo na Biden

Image
  Rais wa Marekani Joe Biden amemwambia waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba "inaonekana" "shambulio la hospitali ya Al Ahli lilitekelezwa na kundi jingine ". Biden anasema "amehuzunishwa sana na kukasirishwa" na tukio hilo. "Kulingana na kile nimeona inaonekana kana kwamba shambulio hilo lilitekelezwa na kundi jingi, sio wewe. Lakini kuna watu wengi huko nje ambao hawana uhakika, kwa hivyo lazima tukabiliane na mambo mengi," alisema. BBC inajaribu kuunganisha vipande vidogo vidogo vya mlipuko wa hospitali ya jana usiku - ambao Hamas na mamlaka ya Palestina wanailaumu Israel kwa kutekeleza shambulio la angani. Rais Biden anasema alitembelea Israel ili kuonyesha mahali Marekani iinaunga mkono katika mzozo huo. Anaendelea kuelezea mauaji ya Hamas tarehe 7 Oktoba. Anasema "siyo sifa " kusema "walichinja" watu 1,300, ikiwa ni pamoja na Wamarekani 31. Pia alizungumzia kuhusu mateka wa Israeli, pamoja na watoto. "Heb...

Melodic Techno & Progressive House Mix Olaroch

Image

Urusi imepiga marufuku kwa muda mauzo ya mafuta kwa nchi nyingi kukabili uhaba

  Urusi imepiga marufuku kwa muda mauzo ya petroli na dizeli kwa nchi zote za nje ya mzunguko wa mataifa manne ya zamani ya Soviet na athari ya haraka ili kuleta utulivu wa soko la ndani, serikali ilisema siku ya Alhamisi. Ilisema marufuku hiyo haitumiki kwa mafuta yanayotolewa chini ya makubaliano ya kiserikali kwa wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Eurasia inayoongozwa na Moscow, ambayo inajumuisha Belarus, Kazakhstan, Armenia na Kyrgyzstan. "Vikwazo vya muda vitasaidia kueneza soko la mafuta, ambalo litapunguza bei kwa watumiaji," ilisema taarifa ya serikali. Wizara ya nishati ilisema hatua hiyo itazuia usafirishaji usioidhinishwa wa mafuta ya gari. Marufuku hiyo ni ya muda usiojulikana na hatua zaidi zitategemea soko, kulingana na Naibu Waziri wa Nishati wa Kwanza wa Urusi Pavel Sorokin. "Tunatarajia kuwa soko litakuwa na mabadiliko haraka na ya kutosha. Lakini itategemea soko na matokeo," Sorokin alisema. Urusi katika miezi ya hivi karibuni imekumbwa na uhaba ...

DP WORLD NI NINI

  DP World   ni   kampuni   ya kimataifa ya   Emirati   inayojihusisha na usafirishaji iliyoko   Dubai ,   Falme za Kiarabu . Imejikita na usafirishaji wa mizigo, shughuli za   bandari , huduma za baharini na maeneo ya biashara huria. Iliundwa mwaka   2005   kwa muunganiko wa mamlaka ya bandari ya Dubai ( Dubai Ports Authority ) na mamlaka ya bandari ya Dubai kimataifa ( Dubai Ports International ), DP World inashughulikia   makontena   milioni 70 ambayo huletwa na karibu   meli   70,000 kila mwaka. Hii ni sawa na takriban 10% ya makontena yanayosafirishwa ya kimataifa yanayotolewa na vituo vyao 82 vya baharini na nchi kavu vilivyopo katika zaidi ya nchi 40. Hadi mwaka   2016 , DP World ndiyo kampuni iliyokuwa ikiendesha bandari kimataifa, na tangu wakati huo, imepata na kushirikiana na makampuni mengine juu na chini ya mnyororo wa thamani. Historia [ hariri  |  hariri chanzo ] Zamani [ hariri ...

Kwa nini Japan ndiyo nchi yenye madeni zaidi duniani?

  Mwishoni mwa Septemba mwaka jana, Japan ilikuwa inakaribia takwimu ambayo ingesababisha kuzizimz katika nchi nyingine yoyote duniani na kwamba, mbali na kukaa huko, itaendelea kukua katika siku zijazo. Deni lake la umma lilifikia dola za Marekani trilioni 9.2, ambayo ni, 266% ya Pato la Taifa, juu zaidi ikilinganishwa na nchi nyingine. Kwa kulinganisha, ile ya Marekani ilifikia dola za Marekani trilioni 31 katika kipindi hicho, lakini kutokana na ukubwa wa mamlaka inayoongoza duniani, kiasi hiki ni sawa na asilimia 98 tu ya Pato la Taifa. Sababu ya idadi hiyo kubwa ni kwamba nchi imetumia miongo kadhaa kuongeza matumizi ya ndani ili kuufanya uchumi wake uendelee. Raia wake na biashara, ambazo zina jukumu muhimu katika ukuaji wa uchumi, wanasita sana kutumia na serikali mara nyingi hulazimika kutumia kwa ajili yao. "Akiba ya binafsi ni kubwa na uwekezaji ni dhaifu, ikimaanisha mahitaji dhaifu," anasema Takeshi Tashiro, mwandamizi katika Taasisi ya Peterson ya Uchumi wa Kimat...