Posts

Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi

Kwa nini Jordan ilikosolewa baada ya mashambulizi ya anga ya Iran dhidi ya Israel?

Image
CHANZO CHA PICHA, REUTERS 18 Aprili 2024 Uamuzi wa Jordan wa kuunganisha nguvu na Marekani, Uingereza na Ufaransa kuzuia ndege zisizo na rubani na makombora yaliyorushwa na Iran dhidi ya Israel usiku wa Aprili 13 ulikabiliwa na hisia kali ndani ya nchi na eneo hilo. Baada ya kauli za vitisho ya Tehran, Amman alimuita balozi wa Iran siku ya Jumapili. Shirika la habari la Fars liliripoti kwamba vikosi vya jeshi la Iran "vilikuwa vinafuatilia kwa makini mienendo ya Jordan wakati wa mashambulizi ya kuadhibu dhidi ya utawala wa Kizayuni" na kuonya kwamba Jordan itakuwa "shabaha inayofuata" ikiwa itaingilia kati. Jordan, ambayo inapakana na Israel, ndiyo nchi inayohifadhi idadi kubwa zaidi ya Wapalestina na kihistoria imekuwa ikionekana kuwa mfuasi wao mkubwa katika eneo hilo. Mfalme Abdullah, kiongozi wa nchi hiyo ambaye ana mtazamo wa kukosoa vita vya Gaza, aliunga mkono waziwazi juhudi za kupeleka misaada katika eneo hilo kwa njia ya anga. CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGE

Urusi inatengeneza silaha mpya ya kushambulia satelaiti - Marekani

Image
  CHANZO CHA PICHA, EPA Maelezo ya picha, Wataalamu waliambia BBC kwamba silaha yoyote inaweza kusababisha machafuko kwa tegemeo la setilaiti ya Marekani (picha ya faili) 16 Februari 2024 Urusi inatengeneza silaha mpya ya kupambana na satelaiti, Marekani imesema, lakini ilisisitiza kuwa Moscow bado haijaitumia. Msemaji wa Ikulu ya Marekani John Kirby alitoa maoni hayo siku moja baada ya mjumbe mkuu wa chama cha Republican kutoa onyo lisilo wazi la "tishio kubwa la usalama wa taifa". Silaha hiyo ni ya anga za juu na ina silaha ya nyuklia kulenga satelaiti, mshirika wa BBC wa Marekani CBS News aliripoti. Lakini Bw Kirby hakuthibitisha hili na alikataa kutoa maelezo sahihi kuhusu tishio hilo siku ya Alhamisi. Moscow iliishutumu Marekani kwa kutumia madai ya silaha mpya za Kirusi kama mbinu ya kulazimisha Bunge la Congress kupitisha msaada wa ziada wa Ukraine kwa "kivyovyote vile ". Bw Kirby, ambaye hivi majuzi alifanywa msaidizi mkuu wa Rais Joe Biden, aliwaambia waand

Edward Lowassa afariki dunia

Image
  Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa amefariki dunia, akiwa anapatiwa matibabu jijini Dar es Salaam. Tangazo la kifo cha Lowassa kimetangazwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango. Katika tangazo fupi alilolitoa kupitia televisheni ya taifa, Mpango amesema kuwa Lowassa amefikwa na umauti katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Lowassa alihudumu kama Waziri Mkuu wa Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa miaka mitatu, toka 2005 mpaka 2008 alipolazimika kujiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia hii leo. Mwaka 2015 Lowassa alikihama chama tawala cha CCM baada ya kukosa tiketi ya kuwania urais kupitia chama hicho. Alitimkia chama kikuu cha upinzani cha Chadema ambapo aliungwa mkono kugombea urais na vyama vilivyounda umoja wa upinzani wa UKAWA kwa wakati huo. Lowassa hata hivyo alishindwa katika uchaguzi huo na aliyekuwa mgombea wa CCM J

Netanyahu akataa mapendekezo ya Hamas ya kusitisha mapigano Gaza

Image
CHANZO CHA PICHA, SERIKALI YA ISRAEL Saa 6 zilizopita Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekataa mapendekezo ya Hamas ya kusitisha mapigano - akisema "ushindi kamili" huko Gaza unawezekana ndani ya miezi kadhaa. Alikuwa akizungumza baada ya Hamas kuweka msururu wa matakwa kujibu pendekezo la kusitisha mapigano lililoungwa mkono na Israel. Bw Netanyahu alisema mazungumzo na kundi hilo "hayaendi popote" na akaelezea masharti yao kama "ya kustaajabisha". Mazungumzo yanaendelea kujaribu kufikia makubaliano ya aina fulani. "Hakuna suluhu lingine ila ushindi kamili na wa mwisho," Bw Netanyahu aliambia mkutano wa wanahabari Jumatano. "Ikiwa Hamas itasalia Gaza, ni suala la muda tu hadi mauaji yajayo." Israel ilitazamiwa kukabiliana na pendekezo la Hamas, lakini jibu hili ni kama kukemea, na maafisa wa Israel wanaona wazi juhudi za Hamas kumaliza vita kwa masharti yake kama jambo lisilokubalika kabisa. Afisa mkuu wa Hamas Sami Abu Zuhri