Posts

Showing posts from April, 2025

Trump aitaka Iran kuingia makubaliano ya nyuklia, akionya kuhusu mashambulizi ya kikatili zaidi

  Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Iran kufanya makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia, akisema aliipa Tehran nafasi baada ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kuhusu makubaliano yalikuwa yanakaribia kuingia awamu ya sita Jumapili. "Niliwaambia, kwa maneno makali, "fanyeni tu," ingawa walijaribu sana, haijalishi walikuwa karibu vipi, hawakuweza kufanikiwa," Trump anaandika kwenye mtandao wa kijamii wa Truth. "Iran lazima ifanye makubaliano na kuokoa kile ambacho hapo awali kilijulikana kama Dola ya Iran. Hakuna kifo tena, hakuna uharibifu tena, FANYA TU, KABLA HAMJACHELEWA." Hapo awali Trump alisema anafahamu mipango ya Israel kabla ya kuanza mashambulizi usiku kucha, lakini aliweka wazi kuwa wanajeshi wa Marekani hawakushiriki katika operesheni hiyo.

Tundu Lissu afikishwa Mahakamani asomewa shitaka la uhaini

Image
  Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini tanzania, Chadema, Tundu Lissu jioni hii amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, na kusomewa shitaka moja la uhaini. Tundu anayetetewa kwa sasa na Mawakili sita ambao ni Dk. Rugemeleza Nshalla, Dickson Matata, Jebra Kambole, Michael Lugina, Hekima Mwasipu, na Gaston Garubindi, alisomewa shitaka hilo la Wakili Nassoro Katuga Awali Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilisema lilimkamata Lissu jana mkoani Ruvuma kwa tuhuma za kufanya uchochezi wa kutofanyika Uchaguzi Mkuu 2025. Aidha Polisi nchini humo kupitia taarifa yake ilitoa onyo kwa vyama vyote vya siasa kutotoa maneno ya uchochezi, kashfa kwa Polisi na Serikali au viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu. Mapema Polisi walipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema huku wakizua viongozi wa chama hicho kufanya mkutano na waandishi wa habari. Vyombo vy...