Posts

Showing posts from June, 2024

Trump aitaka Iran kuingia makubaliano ya nyuklia, akionya kuhusu mashambulizi ya kikatili zaidi

  Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Iran kufanya makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia, akisema aliipa Tehran nafasi baada ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran kuhusu makubaliano yalikuwa yanakaribia kuingia awamu ya sita Jumapili. "Niliwaambia, kwa maneno makali, "fanyeni tu," ingawa walijaribu sana, haijalishi walikuwa karibu vipi, hawakuweza kufanikiwa," Trump anaandika kwenye mtandao wa kijamii wa Truth. "Iran lazima ifanye makubaliano na kuokoa kile ambacho hapo awali kilijulikana kama Dola ya Iran. Hakuna kifo tena, hakuna uharibifu tena, FANYA TU, KABLA HAMJACHELEWA." Hapo awali Trump alisema anafahamu mipango ya Israel kabla ya kuanza mashambulizi usiku kucha, lakini aliweka wazi kuwa wanajeshi wa Marekani hawakushiriki katika operesheni hiyo.

Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi ...