Posts

Showing posts from January, 2023

Israel na Hezbollah wakaribia kupigana, wote wakataa kurudi nyuma

Image
  CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Israel 23 Juni 2024 Vita kamili kati ya Israel na Hezbollah vitasababisha "janga", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema. Lakini kwa David Kamari, ambaye anaishi chini ya moto unaokaribia kila siku upande wa mpaka wa Israel, vita hivyo vitakuwa suluhu. Mwezi uliopita, roketi ya Hezbollah iliyorushwa kutoka Lebanon ilitua kwenye bustani yake katika mji wa mpakani wa Kiryat Shmona, na kupasua nyumba yake katika maeneo kadhaa na kuijaza na vifusi. Anaonyesha mashimo ambayo vipande vya misumari vilipita kwenye kuta, vikimkosa kwa inchi chache. Na kisha kwenye vilima vilivyo juu yetu, ambapo eneo linalodhibitiwa na Hezbollah linaanzia. "Kila siku, kila usiku: mabomu. [Ni] tatizo," alisema. "Na mimi nilizaliwa hapa. Ikiwa unaishi hapa usiku mmoja, utakuwa na wazimu." David bado anaishi katika nyumba yake iliyojaa vifusi, vipande vya misumari vilivyonaswa na mabaki ya televisheni yake. Nje ni masalio meusi

Kwa nini Japan ndiyo nchi yenye madeni zaidi duniani?

  Mwishoni mwa Septemba mwaka jana, Japan ilikuwa inakaribia takwimu ambayo ingesababisha kuzizimz katika nchi nyingine yoyote duniani na kwamba, mbali na kukaa huko, itaendelea kukua katika siku zijazo. Deni lake la umma lilifikia dola za Marekani trilioni 9.2, ambayo ni, 266% ya Pato la Taifa, juu zaidi ikilinganishwa na nchi nyingine. Kwa kulinganisha, ile ya Marekani ilifikia dola za Marekani trilioni 31 katika kipindi hicho, lakini kutokana na ukubwa wa mamlaka inayoongoza duniani, kiasi hiki ni sawa na asilimia 98 tu ya Pato la Taifa. Sababu ya idadi hiyo kubwa ni kwamba nchi imetumia miongo kadhaa kuongeza matumizi ya ndani ili kuufanya uchumi wake uendelee. Raia wake na biashara, ambazo zina jukumu muhimu katika ukuaji wa uchumi, wanasita sana kutumia na serikali mara nyingi hulazimika kutumia kwa ajili yao. "Akiba ya binafsi ni kubwa na uwekezaji ni dhaifu, ikimaanisha mahitaji dhaifu," anasema Takeshi Tashiro, mwandamizi katika Taasisi ya Peterson ya Uchumi wa Kimat